Tuesday, August 30, 2011

EID MUBARAQ

Hello Tanzanian!
We would like to share Eid Mubarak  to all of you and welcome all of you to share with us Eid celebration at our attractive zoo at affordable cost for your enjoyment.
Dar es Salaam Zoo has now established seven (7) spacious gardens with adequate day time accommodation to hold Group/Family Celebrations at reasonable costs.  This is apart from the pleasure of enjoying the natural fresh environment, the direct interaction with wildlife and the excitement of recreation celebrities provided at the zoo such as horse/camel riding and motor cycle/go-cart racing in and outdoor games like football, tennis and volleyball .  We just open u horse club with affordable fee to be a membership .


Salim Hassan
Marketing Manager










Friday, August 26, 2011

Walipa Kodi 15 Bora

Mheshimiwa Spika,

1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:

i.              Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);

ii.            National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii.           Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv.            National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v.            CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi.           Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii.          Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii.        Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

ix.           Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x.            Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi.           Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii.          Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii.        Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv.         Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv.          Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).

2.  Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria

Zitto aibua tuhuma nyingine dhidi ya Serikali

SERIKALI na Bunge zimeingia katika mkwaruzano mwingine baada ya Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, kuituhumu Serikali kuwa imemsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi (CHC), Mathusela Mbajo, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuvujisha siri za Serikali kwa Bunge.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa tuhuma hizo jana wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2011/2012.Juzi Bunge liliingia katika mvutano na Serikali baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo, bila Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kujadiliwa bungeni.

Kabla sakata hilo halijapoa, Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alidai kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya Mbajo ni matokeo ya Azimio lililopitishwa na Bunge kuliongezea shirika hilo muda.

"Baada ya kufanya marekebisho hayo, azimio lililopelekwa na Serikali bungeni likiwa na nia ya kuunganisha shirika hilo na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Zitto alisema uamuzi huo wa Bunge haukuwafurahisha baadhi ya watendaji wa Serikali hivyo ikaamuliwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu huyo wa CHC, kwa tuhuma zilizojaa majungu kutoka kwa wanaojiita wafanyakazi wa CHC," alisema Zitto na kuongeza.

"Tuhuma hizo ziliwasilishwa kwangu binafsi na kunakiliwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Kufuatia maagizo ya Waziri wa Fedha kwa Bodi ya Wakurugenzi wa CHC, Mtanzania huyu akasimamishwa kazi na CAG ameombwa kuchunguza majungu yale kutoka kwa wanaojiita wafanyakazi wa shirika hilo.

"Mheshimiwa Spika, nilikuandikia barua kukuomba hatua mwafaka zichukuliwe, kwani suala hili bado lipo katika mamlaka ya Bunge na kwa mujibu wa Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sheria namba 3 ya mwaka 1988, uamuzi huu Waziri wa Fedha ni sawa na kulidharau Bunge"

Waziri kivuli huyo aliongeza: "Barua ya wanaojiita wafanyakazi wa CHC (niliyoandikiwa Juni 24, 2011, siku mbili tangu kupitishwa kwa azimio la Bunge na kuwatuhumu mawaziri kuwa walishawishiwa), Barua ya maelekezo ya Serikali (iliyosainiwa na ndugu Mmbaga, Msaidizi wa Waziri Mkuu ya tarehe 10 Agosti 2011) na barua yangu ya majibu (18 Agosti 2011) niliyowapa, zimewasilishwa mezani kwako kama vithibitisho na kwa hatua zaidi utakazoona inafaa."

Zitto aliliomba Bunge kusimama imara ili kuzuia kuingiliwa kwa mamlaka yake na tawi la utendaji kwa kuwa mijadala ndani ya Bunge inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo lisipokuwa makini Bunge litaendelea kudharauliwa hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali ipasavyo.

"Ninataka maelezo ya kina ya Waziri wa Fedha kwa nini amechukua hatua nilizoeleza hapo wakati akijua jambo hili lipo mezani kwa Spika wa Bunge."

Usimamizi wa mashirika ya Umma
Katika eneo hilo, Zitto aliituhumu Serikali kwa kushindwa kusimamia hisa zake katika makampuni akieleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) imekuwa dhaifu mno katika kusimamia mali za umma katika mashirika na kutoa mfano wa hisa za kampuni ya Oryx na Tigo.

"Kampuni ya Oryx ilikuwa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 50 mpaka mwaka 2004. Mwaka 2004, kupitia ofisi ya TR Serikali iliuza hisa zake ambazo ni asilimia 50 kwa bei ya kutupa kwa thamani ya dola 2.5 milioni. Hivi sasa Oryx ni moja ya kampuni inayofanya vizuri sana katika sekta ya mafuta, lakini hatuna umiliki tena na pesa kiduchu tulizopata zimekwishatumika," alisema Zitto na kuongeza:

"Pia Serikali ilikuwa na hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel ambayo kwa sasa inajulikana kama “tigo”. Katika hatua ya kushangaza Serikali imeuza hisa zake asilimia 16 kwa thamani ya Dola 1.3 milioni mwaka 2006 na kwa sasa kampuni hiyo ni ya kigeni kwa asilimia mia moja jambo ambalo ni kinyume na sheria."
Zitto alisema kampuni za simu zinatakiwa kumilikiwa na Watanzania si chini ya asilimia 35.

Makusanyo ya kodi
Zitto alisema kambi ya upinzani nasikitishwa na pungufu ya makusanyo madogo ya kodi na kwamba, hali hiyo imetokana na Serikali kushindwa kusikiliza maoni yanayotolewa na kambi hiyo kila mwaka ambayo ni vyanzo mbadala vya kuongeza mapato.

Kuhusu bei ya dhahabu

Zitto alifafanua kwamba bei ya dhahabu katika soko la dunia imeongezeka mara dufu na hadi kufikia Agosti 23, mwaka huu. Kwa mujibu wa mtandao wa gold-alert bei ya dhahabu ilikuwa Dola za Marekani 1,902.61.
Alisema hilo ni ongezeko kubwa na hivyo kuna haja ya kuangalia namna ya kurekebisha kodi kwenye madini hayo ili taifa lifaidike na bidhaa hiyo.

Kutokana na ongezeko hilo la bei, alisema kambi ya upinzani inaitaka Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) kuanza mara moja kufanya utafiti wa namna bora ya kutoza kodi ya faida kwenye dhahabu (windfall tax), ili kuongeza mapato ya Serikali kwa sababu wawekezaji wanapata faida mara dufu kwa sasa.

"Matokeo ya tafiti hii yaletwe bungeni kama muswada wa sheria ili kurekebisha sheria za kodi na kutoza aina hii mpya ya kodi," alisema Zitto

Alisema kambi ya upinzani inapendekeza kwa kuwa gharama ya kuzalisha wakia moja ya dhahabu hapa nchini ni wastani wa dola za marekani 650, basi bei ya dhahabu ikiwa ya kati ya dola 1,000 – 1,300, mrabaha uwe mara mbili ya tozo za sasa.

"Kwa mfumo huu, taifa litafaidika na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia na pale ambapo bei zitashuka wawekezaji watalipa mrabaha wa kawaida," alifafanua aziri kivuli huyo.

Alisema iwapo mfumo huo wa kodi katika madini ungekuwa unatumika sasa na ambapo bei ya dhahabu imefikia zaidi ya dola 1,900 kwa wakia, na nchi inazalisha takribani tani 60 ya dhahabu kwa mwaka, Serikali ingekusanya takribani Sh450 bilioni kama mrabaha.

"Hii ingetuwezesha hata kutokopa kwa ajili ya umeme wa dharura kama tunavyoelekea kufanya sasa."

Monday, August 22, 2011

ASEMA KAMA INATAKA KUENDELEA KUSHIKA DOLA IWAFUKUZE WATUMUMIWA WA UFISADI





WAZIRI Mkuu mstaafu, John Malecela amekitaka Chama chake cha Mapinduzi (CCM) kuwachukulia hatua za haraka wala rushwa walioko ndani yake kuanzia ngazi ya juu hadi chini kama kinataka kuendelea kushika dola.Kauli ya Malecela ambaye ni Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, inakuja kipindi ambacho mpango mkakati wa chama hicho wa kujivua gamba unaonekana kupigwa kalenda.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Sea View, Upanga Dar es Salaam jana, Malecela alisema ni muhimu wala rushwa wakaondolewa haraka bila kucheleweshwa ili chama kiendelee kuwapo.

Malecela alinukuu maandiko ya Mungu katika Ukristo akisema: "Mimi ni Mkristo, maneno ya Mungu yanasema ukiwa na jicho bovu na ukiona linakuzuia kuingia mbinguni litoe ili uweze kuingia."

"Kama kuna corrupt people in the party (wala rushwa ndani ya chama), ni kuwaondoa ili CCM iendelee kuwapo."

Hata hivyo, alisema suala la kujivua gamba haliwezi kuwa kwa watu wanne au watano, bali chama kisafishe wala rushwa wote waliopo ndani yake kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Kujivua gamba
Mpango wa kujivua gamba kwa CCM ulianza kutangazwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa chama hicho yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni akisema yalikuwa na lengo la kukihuisha.

Rais Kikwete alisema chama hicho kiliwahi kufanya mabadiliko mbalimbali kuanzia TANU kwa lengo la kujisafisha na kujipanga upya, baada ya kujifanyia tathmini kuhusu mwelekeo wake kwa wakati husika.

Mpango huo baadaye ulijadiliwa katika CC iliyokutana Mjini Dodoma mnamo Aprili ambayo pamoja na mambo mengine utekelezaji huo ulianza kwa Kamati hiyo Kuu kujiuzulu yote na kusukwa upya huku baadhi ya watuhumiwa akiwamo Andrew Chenge kutupwa nje.

Katika kikao hicho, ilitangazwa watuhumiwa wa ufisadi ukiwamo wa Richmond, Rada na Kagoda iliyochota Sh40 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wangepaswa kujipima na kuachia nafasi zao ndani ya siku 90 lakini hadi kikao cha CC cha mwezi uliopita, watuhumiwa hao walikuwa hawajajiuzulu.

Badala yake, CC ilitoa muda zaidi kusubiri uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho inayotarajiwa kukutana mwezi ujao.Hata hivyo, hakuna dalili zozote za watuhumiwa wakubwa wanaotajwa katika kashfa hizo za rada na Richmond kujiuzulu huku chama kikionekana kuwa katika wakati mgumu kuwafukuza, huku hatua ya kutowafukuza ikitajwa kama kitanzi kinachoweza kukimaliza kisiasa.

Tuhuma za kumiliki shamba hekta 100
Akizungumzia madai yaliyotolewa Bungeni hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kwamba anamiliki hekta 100 za shamba huko Mvomero, Morogoro, Malecela alisema hana habari juu ya umiliki huo akisema: "Sina hati yake na wala sijawahi kufika kuliona, hata sijui liko sehemu gani ya Mvomero."

Alisema wakati Serikali ilipoipa Mvomero hadhi ya wilaya, iliwapa baadhi ya viongozi mashamba ili waendeleze maeneo hayo au wavute wawekezaji katika wilaya hiyo."Mimi niliambiwa nimepewa hekta 100 lakini sijawahi kufika kwenye eneo hilo, hata hati ya shamba hilo sina hivyo ni kusema sina shamba Mvomero."

"Ambaye analitaka shamba hilo akalichukue au kama kuna mtu anayefikiri kuwa ana hati ya shamba hilo aende wizarani athibitishe."

"Ni miaka 10 imepita tangu niambiwe suala hilo, wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akiwa ni (Samwel) Kamote, lakini sheria za kutoendeleza mashamba si zinajulikana kama lipo tu kwa nini lisichukuliwe?"

Malecela alisema asingeweza kupeleka trekta kutoka Dodoma kwenda kulima Mvomero hekta 100 kwa kuwa uwekezaji unahitaji zaidi ya hekta 300.

Alichokisema Mdee bungeni
Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), akisoma bajeti mbadala ya upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2011/12 aliwataja baadhi ya viongozi wa CCM wakiwamo Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa akiwatuhumu kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro huku wakishindwa kuyaendeleza. Hata hivyo, Mkapa anaelezwa kuendeleza shamba lake.

Katika orodha hiyo pia ametajwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula, aliyekuwa Naibu wake (Tanzania Bara), Hassan Ngwilizi na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawab Mulla.

Mdee alisema umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi unawanyima fursa wananchi wa kawaida kupata maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza kwamba, vigogo hao kwa kutumia nafasi zao waliwanyang’anya wananchi ardhi hiyo na kujimilikisha wenyewe lakini kwa sehemu kubwa wameshindwa kuyaendeleza.

“Mheshimiwa Spika, matatizo ya ardhi kwa wakubwa kunyang’anya wanyonge imekumba pia Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambako mgogoro huu unakumba shamba namba 299 iliyokuwa Narco Ranches lenye ukubwa wa hekta 49,981," alisema na kuongeza:

“Taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa maeneo yaliyokuwa yamepangwa kugawiwa kwa wanavijiji wa Kijiji cha Wami, yamegawiwa wanavijiji wafuatao,’’ alisema na kuanza kuwataja vigogo hao kwa majina mmoja baada ya mwingine.

Akitoa orodha hiyo, Mdee alisema  Mangula anamiliki hekta 2,000, Mwinyi hekta 2,000 na Mkapa hekta 1,000 ambaye hata hivyo, ndiye pekee aliweza kuliendeleza shamba lake.

Katika orodha ya Mdee alimtaja pia  Sumaye kwamba anamiliki hekta 500, Malecela hekta 100 na Ngwilizi ambaye anamiliki hekta 100 huku akisisitiza orodha hiyo ni ndefu.Mdee alitaka Serikali itoe maelezo kwamba ni vigezo vipi vilitumika kuwagawia ardhi viongozi hao huku wakiwanyima ardhi wananchi wa maeneo husika.

Jembe jipya darajani


Matajiri wa londo Chelsea fc wamekubaliana na Mchezaji Juan Mata pamoja na Club ya valencia ya Uhispania ada ya Uhamisho ya Pound 26ml na kumnyakua mchezaji huyo kwa ajili ya msimu huu wa ligi.

Wambea tafuteni Kivuri Jua kali Mwaka Huu




Mtu Mweusi Mboga Asia

ONYO - Nimepata kwa email. Kama huna roho ngumu usiangalie hizi picha! Kama sikosei ni Thaliand hapo. Cheki wanavyomkata huyo marehemu kama nyama kwenye bucha! Nadhani tumejua ndugu zetu walioenda huko na wakapotea waliishia wapi sasa! DUH!



















Email Text:
THAI & CHINESE PEOPLE EATING A BLACK MAN. I have never seen anything like this before! The Asian appetite for "exotic" taste sometimes scare me - from stories of cat eating to dogs, to lizard, snakes to all sorts of crazy fish, then human embryos and now to fully grown humans! The photo of the person you are about to watch could have been somebody's fiance, husband or Dad! This looks too real to be true.
How I wish all black leaders watch these photos and give guidelines of who they allow to migrate into their countries. The time has come for black (Africans, American, West Indies etc) to rise and unite together against attrocities committed by foreigners on them either on their soil or abroad. Time to pray to God is now!

Mbunge Apata ajali Dodoma

Mbunge kutoka baraza la wawakilishi, Mh. Mussa Hamisi Silima apata ajali Dodoma jana jioni akitokea Dar es salaam kuelekea Dodoma akiwa na familia yake. Kwa mujibu wa Spika Anne Makinda, Mkewe Mwanaheri Fahari, amefariki dunia. Mh Silima alikuwa ametokea zanzibar kwenye mazishi. 
Maiti na Majeruhi wanatarajiwa kusafirishwa asubuhi hii kwa ndege kwenda Zanzibar.
Mola aiweka Roho ya marehemu mahali pema peponi na awajaalie walioheruhiwa kupata ahueni haraka

Sunday, August 21, 2011

Wazee wa DArajani waanza Kazi EPL

Flank Lampard Akifanyiwa madham,bi wakati akijaribu kuwahadaa mabeki wa West Brom

Timu ya Chelsea fc ya Jijini London Jana ilianza Ubabe wake kwa kuibugiza timu ya West brom Albion Mabao Mawili kwa moja,
Chelsea ikitokea nyuma ili sawazisha goli kupitia kwa Mkongwe Nicolas Anelkana lile la ushindi likishindiliwa kimiani na Flo maluda.
Florent Malouda akikazia swaum kwa Bao Malidadi la ushindi






Tuesday, August 16, 2011

Aguero ampa kiburi Mancini

The £38million striker came off the bench after Edin Dzeko's opener to tap home No 2, brilliantly set up David Silva for the third then crack in a 30-yard humdinger.

JOY ... but Mancini wants more
JOY ... but Mancini wants more
Mancini said: "He needs another two or three weeks to be 100 per cent. "He has worked only one week with the team and he needs to improve. He has to recover from the Copa America three weeks ago.
"He's a fantastic striker, he's young and he will be a fantastic player for us in the future.
"He linked very well with David Silva - they play in the same language.
"I'm delighted after this performance.
"I thought in the first half Swansea played very well.
"But after 25 minutes we started to press and had many chances to score.
"It is only the first match - the season will be long.


"But it was very important for us to start like this."
After the match, Aguero took to Twitter to express his delight at his performance.
He said: "Very happy with my debut for City. Hopefully the start of something big. Thank you to my team-mates and the fans for their support."
And his team-mates were cock-a-hoop at the 23-year-old's dream debut.
City goalkeeper Joe Hart said: "He's decent isn't he?
"He came with a big price tag, but it's money well spent."
And skipper Vincent Kompany added: "He has definitely come as a surprise.
"He has great potential and the most important thing for me is that you saw some moments of him defending and working hard.
"For us, for the team this season, that's important."
Swansea manager Brendan Rodgers was far from dismayed despite the scoreline.
 He said: "I'm very proud of my team because up until the hour mark we were fantastic, had good possession and we looked like we could create something.
"But we conceded two quick goals and after that it was very difficult.
"There's a fantastic spirit in the group. It wasn't an ideal result but we'll take many positives from it.
"We won't be downhearted. We will continue to play the way we play and we know we won't come up against this quality of opposition every week."

Kashfa nyingine ya posho yatua kwa Ngeleja, Malima

Waziri Ngeleja na Malima wakiwa Bungeni
 WADAIWA KUPATA MGAWO WA SH 4 MILIONI KILA MMOJA FEDHA ZILIZOKUSANYWA NA JAIRO
Mwandishi Wetu
TUHUMA zilizosababisha kupelekwa likizo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo zimezidi kupanuka na sasa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima wanadaiwa kupokea sehemu ya fedha zilizosababisha mtendaji huyo kupewa likizo ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

Jairo yupo likizo baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuanzisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa bungeni kwamba aliwaandikia barua wakuu wa idara chini ya wizara yake ili watoe fedha kusaidia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, fedha ambazo zinatafsiriwa kwamba zililenga kuwahonga wabunge.

Lakini wakati umma wa Watanzania ukisubiri hatima ya Jairo huku suala lake likiwa bado halijafikia mwisho, imebainika kuwa Ngeleja na Malima kila mmoja alinufaika na mgawo wa fedha hizo kwa kila mmoja kupewa kiasi cha Sh4 milioni, kwa maelezo kwamba ni fedha za kuwakirimu wageni.

Imeelezwa kuwa kiasi cha fedha kilichokusanywa na Jairo na kuingizwa katika akaunti ya Tanzania Geological Survey (GST), namba 5051000068 kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma ni Sh460 milioni na siyo bilioni moja kama ilivyodaiwa awali.

Hesabu kwamba fedha hizo zingefikia Sh1 bilioni ilitokana na barua iliyosomwa bungeni na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambayo ilikuwa ikibainisha kwamba fedha zilizoombwa ni Sh50 milioni, ambazo zikizidishwa kwa idadi ya idara na taasisi 21 zilizopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini zinaleta jumla hiyo ya kiasi cha fedha.

Mwandishi wa gazeti hili aliona dokezo la Julai 16, mwaka huu la Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Nishati na Madini aliyefahamika kwa jina la I.H. Swai kwenda kwa Jairo likipendekeza kwamba Waziri na Naibu wake wapewe kila mmoja kiasi cha Sh4 milioni kwa ajili ya kuwakirimu wageni: “Hasa katika kipindi hiki cha Bunge la Bajeti.”

Dokezo hilo lilisema: “Kulingana na uzito wa kazi za Wahe. Waziri na Naibu Waziri, nashauri wapewe entertainment allowance ya Sh4 milioni kila mmoja, ili kuwawezesha kubalishana mawazo/kushauriana na wadau muhimu na wananchi wa majimbo yao, wanaofika Dodoma kuwaona kwa masuala mbalimbali ya maendeleo ya majimbo yao, katika kipindi hiki cha Bunge la bajeti.”

Dokezo hilo liliidhinishwa na Katibu Mkuu, Jairo Julai 18, 2011 kwa kuandika neno “Sawa” kisha kulisaini ikiwa ni kukubaliana na mapendekezo ya Swai na siku hiyo fedha hizo kiasi cha Sh8 milioni kililipwa kwa wahusika.

Hata hivyo, maelezo ya dokezo hilo yanatofautiana na yale yaliyo kwenye fomu iliyotumika kwa ajili ya kufanya malipo hayo ambayo inasomeka “Fomu ya Malipo ya Entertainment Allowance kwa ajili ya wajumbe kuwezesha uwasilishaji wa hotuba ya bajeti kwa mwaka 2011/12.”

Chini ya kichwa hicho kuna neno tarehe........ ikiacha nafasi wazi kwa ajili ya kujaza tarehe ambayo malipo hayo yalifanyika na katika fomu ya malipo ya Ngeleja na Malima imeandikwa 18/7/2011.

Kwa mujibu wa fomu hiyo ya malipo, waliochukua fedha hizo Julai 18, 2011 ni wawakilishi wa viongozi hao ambao mmoja ametakwa kwa jina moja la Massola kwa niaba ya Ngeleja na mwingine aliyefahamika kwa jina la E. Shija aliyesaini fedha hizo kwa niaba ya Malima. Msaidizi wa Waziri Ngeleja anaitwa Sosthenes Massola, wakati msaidizi wa Malima anajulikana kwa majina ya Emmanuel Shija.

Julai 18, mwaka huu ni siku ambayo Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliamua kuiondoa bungeni Hotuba ya Bajeti ya Nishati na Madini baada ya wabunge karibu wote waliopata fursa ya kuchangia kukataa kuunga mkono, hadi iliporejeshwa bungeni Agosti, 13 mwaka huu na kupitishwa baada ya Serikali kuwasilisha mpango wa dharura wa kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Bajeti ya wizara hiyo iliwasilishwa bungeni Ijumaa, Julai 15, 2011 na wabunge wengi waliopata nafasi ya kuchangia walieleza wazi kwamba hawako tayari kuiunga mkono kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa zikigusa sekta za madini na umeme.

Taarifa za awali za kiuchunguzi zilidokeza kuwa siku moja baadaye (Jumamosi, Julai 16, 2011) na Jumatatu Julai 18, 2011 kilichukuliwa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika akaunti ya GST, hali iliyozua maswali kuhusu mtiririko huo wa utoaji wa fedha.

Akaunti hiyo ndiyo iliyotumika kukusanya fedha kutoka katika taasisi mbalimbali zilizoko chini ya Wizara ya Madini kwa ajili ya kile kilichodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya wizara bungeni.

Uchukuaji wa fedha nyingi ulizua hoja na wasiwasi kwamba huenda madai kwamba hakukuwa na nia njema ya matumizi ya fedha hizo yalikuwa ya kweli.

"Wachunguzi wetu wanajenga hoja hapa kwamba kwa nini fedha hizi nyingi zilichukuliwa Jumamosi baada ya mambo ya wizara kuonekana kuwa siyo mazuri siku iliyotangulia (Ijumaa)?," kilihoji chanzo chetu na kuongeza kuwa:

"Hata hizi fedha nyingine zilizochukuliwa Jumatatu nazo zina walakini, lazima hapa tuchunguze kwa sababu kuna kitu ambacho siyo cha kawaida."

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, shughuli za kibajeti ni pamoja na posho za vikao (sitting allowance), posho za kujikimu (per diem), ununuzi wa vyakula na vinywaji na gharama za mafuta kwa magari ya watumishi hao.

Ngeleja na Malima

Ngeleja na Malima walipoulizwa kwa nyakati tofauti bungeni Dodoma jana kuhusu madai ya kupewa posho hizo, hawakuthibitisha wala kukanusha.

Ngeleja kwa upande wake alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwani kwa kufanya hivyo ni kama angekuwa “akijitetea” hivyo kutaka suala hilo aulizwe Mkurugenzi wa Mipango ya Wizara yake na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

“Mimi nadhani uwaambie watu wenu wa Dar es Salaam waende pale kwa Mkurugenzi wa Mipango, pale ofisini kwetu ili waweze kupata maelezo, yeye (mkurugenzi) na mhasibu mkuu ndiyo wanaofahamu haya mambo ya posho,” alisema Ngeleja.

Kwa upande wake, Malima alisema suala la msingi ni gazeti hili kufutilia suala la posho za mawaziri na manaibu wao katika Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ili kubaini iwapo wao ndiyo waliolipwa fedha za aina hiyo tu au pia ni kwa mawaziri wengine.

“Mimi nadhani mnatakiwa kuwauliza watu wa Utumishi ili wawaambie maana hapa tunapokuwa bungeni, kuna mambo mengi yanafanyika, sasa ni vizuri mkauliza ili mfahamu waziri na naibu wake ni stahili zipi wanazopaswa kupewa kama allowances (posho),” alisema Malima na kuongeza:

“Maana mnapaswa mjue na muusaidie umma wa Watanzania katika haya mnayoyaandika, kwamba hata kama tulichukua posho hiyo msingi wake ni nini? Halafu jingine kwani ni sisi tu au ni utaratibu wa Serikali kwa mawaziri wake?”

Mhasibu mkuu afafanua
Akizungumzia suala hilo, Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Rose Waniha alisema kuna taratibu zinazotumika katika kutoa posho hizo za kujikimu kwa waziri, naibu na katibu mkuu wawapo katika shughuli maalumu hasa vikao vya Bunge.Waniha alisema kiutaratibu, wakuu wa idara huwa wanafahamu kiasi cha fedha hizo za kujikimu kutegemea aina ya kazi za kiofisi.

"Kwa hiyo hata kunapokuwa na vikao bungeni mtu anayehusika anaangalia labda kila siku waziri au naibu anapaswa kupata kiasi gani cha fedha. Inawezekana ikawa Sh500,000 kwa ajili ya kukirimu wageni . Kwa hiyo hilo dokezo unalolizungumzia ninavyofahamu litakuwa ni la siku za vikao siyo siku mbili ndiyo zilipwe Sh4 milioni kwa mtu mmoja," alisema.

Alipoulizwa kama kuna utaratibu rasmi wa kutoa fedha hizo za kukirimu wageni na viwango maalumu, alisema hakuna viwango maalumu vilivyomo katika dokezo lolote zaidi ya watu wa idara kuangalia uzito wa kazi na idadi ya wageni.

Kuhusu posho ya siku ya kawaida, alisema kwa kawaida waziri, naibu au katibu mkuu anapokuwa safarini, posho ya siku ni Sh80,000 lakini ni tofauti na fedha hizo za kukirimu wageni.

"Posho na fedha hizi za kukirimu wageni ni vitu viwili tofauti. Posho anazolipwa waziri au naibu ni Sh80,000 kama kawaida lakini pesa nyingine za kujikirimu hazina uhusiano na posho," alisema.






























HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MHE. HALIMA JAMES MDEE (MB) KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2010/2011 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MWAKA WA FEDHA 2011/2012

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika
 , napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo kuwasilisha maoni ya Kambi ya upinzani kuhusu Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Spika
, pia nikushukuru wewe kwa kuniruhusu kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara hii kwa mujibu wa Kanuni ya 99 kanuni ndogo ya (7) , ya Kanuni za Bunge Toleo la Mwaka 2007.

Mheshimiwa Spika,
 pili ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na wananchi wa Jimbo la Kawe kwa imani yao kwangu, Makamanda wote (vijana, wazee na akina mama wa vyama vyote) walioshiriki katika harakati zote za Kampeni na hatimaye kukesha na mgombea wao, Shule ya Msingi Oysterbay kulinda ushindi wetu. Mungu pekee ndiye anayejua shukrani yangu kwao! Ahadi yangu kwao, ni kuwatumikia kwa uwezo wangu wote kwa kadiri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha!

Mheshimiwa Spika,
 napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA, Dkt. Wilbroad Peter Slaa. Hakika wabunge wengi tuliofanikiwa kushinda, sehemu ya ushindi ilipatikana kutokana na utumishi wake uliotukuka katika Taifa hili! Mungu akupe uhai,naamini ipo siku tutaifikia Nchi ya Ahadi!

Mheshimiwa Spika,
 sina budi kumshukuru Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mhe. Freemani Aikaeli Mbowe, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa kambi ya Upinzani katika Wizara hii. Shukrani pia ziende kwa wasaidizi wa Kiongozi wa Kambi, Kabwe Zitto (Naibu Kiongozi wa Kambi) na Tundu Lissu (Mnadhimu wa Kambi) kwa kutuongoza vyema katika shughuli hii ngumu ya kuwatetea wanyonge. Shukrani pia ziwafikie wabunge wenzangu wote wa Kambi kwa ushirikiano wao kwangu.

Mheshimiwa Spika, 
sina budi pia kuishukuru sana familia yangu yote,wazazi wangu Prof. James Salehe Mdee na Theresia Kisenga Ngowi kwa upendo wao na kwa upekee nimshukuru kaka yangu Joseph James Mdee, ambaye alikuwa sambaba na mimi, na timu yangu ya kampeni iliyoongozwa na uongozi wa Jimbo la Kawe usiku na mchana mpaka kikaeleweka!

Mheshimiwa Spika,
 mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa kaka yangu na rafiki yangu mkubwa Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Kwa yeyote anayemuona Halima Mdee,na mafanikio yake, afahamu kwamba safari yangu ya mafanikio ya kisiasa yalianzia mbali sana! Na katika safari hii, tokea hatua za awali kabisa, kaka yangu huyu alikuwa mhimili mkubwa. Asante sana.

Mheshimiwa Spika
, ardhi ya Tanzania ina ukubwa wa kilomita za mraba 942,600 sawa na hekta milioni 94.26, kati yake kilomita za mraba 888,200 sawa na hekta milioni 88.82 ni eneo la nchi kavu. Ili ardhi hii iwe na maana katika kuleta maendeleo ni lazima kila kipande kitambiliwe kupimwe, kimilikishwe na kupangiwe matumizi, lakini hadi sasa ardhi iliyopimwa na kumilikishwa inakadiriwa kuwa ni asilimia moja tu. Jambo hili ndilo limepelekea migogoro isiyoisha baina ya watumiaji mbalimbali wa ardhi. Aidha, Serikali kwa makusudi wanapindisha matumizi ya ardhi kwa kuwamilikisha viongozi wa nchi na wafanyabiashara wakubwa kama itakavyojionyesha katika hotuba hii.
Mheshimiwa Spika, asilimia hii finyu ya utambuzi wa ardhi haina maana kuwa ardhi iliyobaki haitumiki au haina mwenyewe, kwani wananchi kwa miaka mingi wamekuwa wakiitumia katika kuendesha maisha yao, hivyo utaratibu wowote unaofanywa na Serikali kuimilikisha kwa mtu yoyote bila kwanza kuhusisha wale watumizi wa awali ni chanzo na kichocheo cha migogoro. Hivyo ardhi iskikodishwe kabla ya kuwafikiria watumiaji wa ardhi hiyo kwenye maeneo husika (wakulima na wafugaji). 
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA ARDHI
Mheshimiwa Spika, Wizara ya ardhi ni wizara mtambuka, chini ya Taasisi yake ya Tume ya Taifa ya Mipango wizara ina wajibu wa kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa mipango na matumizi ya ardhi ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya uwekezaji, kilimo (ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana kwa kwa ardhi kwa ajili ya utekelezaji wa Kilimo kwanza), makazi, malisho (ufugaji), wanyamapori, misitu, vyanzo vya maji na shughuli zote zinazotumia ardhi.

Mheshimiwa Spika,
 Ardhi ndio nchi, Ardhi ndio msingi wa maendeleo. Kwa hiyo hakuna amani,ustawi wala maendeleo kwa wanadamu bila matumizi bora na endelevu ya ardhi. Kwa bahati mbaya, baada ya kukumbatia sera ya uchumi huria ambalo limegeuzwa kuwa holela, uongozi wa nchi yetu umetelekeza kabisa wajibu wa kusimamia matumizi yenye tija ya ardhi kwa nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika, kushindwa huko kumejidhihirisha katika maeneo makuu mawili. Moja, masuala ya usimamizi wa ardhi yamewekwa chini ya Wizara zaidi ya moja hivyo hivyo kuleta mkanganyiko kwenye suala la uwajibikaji. Kuna muingiliano mkubwa sana wa majukumu baina ya Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na ofisi ya waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa ( TAMISEMI). Pili, usimamizi wa maafisa za ngazi za kati na za juu umedhoofika kwa sababu ya kuwajibika kwa zaidi ya mamlaka moja. Mfano halisi ni maafisa ardhi wa halmashauri ya miji na wilaya ambao wanategemewa kuwa chini ya wakurugenzi wa halmashauri na wakati huo huo kuwajibika kwa Kamishna wa Ardhi na Waziri wa Ardhi. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi kutokana na kukosekana kwa usimamizi thabiti wa Maafisa Ardhi.

Mheshimiwa Spika
, takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa halmashauri za wilaya zinaupungufu mkubwa wa wataalam wa ardhi kwa asilimia 74, ikiwa ni sababu mojawapo ya kukua kwa kasi ya ajabu kwa vyombo visivyo na mamlaka kisheria kushiriki katika usimamizi, utawala na kutengeneza matumizi bora ya ardhi ya vijiji kama vile mkuu wa wilaya, mbunge, kamati za ulinzi na usalama na mkuu wa mkoa. Kwa mujibu wa sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999 na ile ya serikali za mitaa namba 7 ya mwaka 1982, hawa hawahusiki na usimamizi wa ardhi za vijiji.

Kambi ya Upinzani
 inaitaka Serikali kueleza mkakati ilionao wa kuviimarisha vyuo vya ardhi vya Tabora na Morogoro ili viweze kutoa wahitimu wengi ili kupambana na upungufu uliopo?
Mheshimiwa Spika, Kutokana na kila taasisi/idara/wizara kujifanyia mambo yake, tumeshuhudia kutupiana mpira baina ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) na Wizara ya Nishati na Madini juu ya mgogoro wa ardhi unaowahusisha wakulima wa kijiji cha Nzasa wakipinga kuondolewa katika makazi yao halali.Katika mgogoro huu Wizara ya Maliasili na utalii wanataka kuwaondoa wananchi katika ardhi yao halali kwa madai kwamba wanaishi ndani ya hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi.

Mheshimiwa Spika, Hifadhi ya Msitu ya wa Kazimzumbwi ilianzishwa na Gavana E.F Twinig kwa Tangazo la serikali Na. 306/1954 la tarehe 24/9/1954. Tangazo hili liliweka mipaka ya Hifadhi ya Misitu wa Kazimzumbwi. Kwa mujibu wa mipaka husika, eneo lililo katika mgogoro halimo katika hifadhi hiyo. Na hata kama lingekuwepo, kwa mujibu wa hukumu za Mahakama utaratibu wa kisheria wa kutangaza eneo kugeuzwa kuwa na hifadhi haukufuatwa hivyo kubatilisha zoezi zima! 

Mheshimiwa Spika, kufuatia malalamiko hayo Ikulu ilimwandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi barua yenye Kumb. Na. CEA 110/302/IV/01 ya tarehe 10/6/2008 ikitaka wizara ikapime eneo la Nzasa- Chanika kujiridhisha kama kweli wakulima hao walikuwa ndani ya msitu wa Kazimzumbwi au la. Barua ambayo haijapatiwa majibu mpaka leo.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaitaka Wizara, iliambie Bunge hili tukufu ni kwa namna gani walifanyia kazi barua toka Ikulu zenye kumbukumbu namba CEA 110 /302/IV/01 ya tarehe 10/Juni 2008 na barua yenye kumbukumbu namba CEA 110/302/IV/01 ya tarehe 18 Septemba 2009 hasa ikizingatiwa kwamba kuna tuhuma kutoka kwa wanakijiji kwenda kuwa viongozi wa serikali ya CCM wanatumia Idara ya Maliasili kama Gamba kutaka kunyang’anya ardhi ya kijiji kwa manufaa yao binafsi. 

MIGOGORO YA ARDHI

Mheshimiwa Spika
,migogoro ya ardhi hapa nchini hivi sasa imekithiri kufikia hatua ya uvunjifu wa amani na kufikia hadi umwagaji damu na pengine vifo kutokea katika maeneo kadhaa. Hali hii imeondoa utamaduni wetu wa asili wa kuvumiliana na kumaliza matatizo yetu kwa njia mwafaka za mazungumzo. Ni muhimu serikali ikaelewa kwamba kupuuzamigogoro hii ya ardhi nchini ni sawa na kuatamia bomu, hivyo ni lazima hatua za haraka zichukuliwe!

UWEKEZAJI, UBINAFISHAJI NA HATMA YA ARDHI YA TANZANIA

Mheshimiwa Spika, Migogoro, hasa ya wananchi na wawekezaji inakua kwa kasi na kuchukua sura mpya. Anapokuja‘mgeni’, kwa jina la ‘Mwekezaji’ matendo ya Serikali yetu, yanapingana na usemi usemao ‘mgeni njoo mwenyeji apone’ bali imekuwa ‘mgeni njoo mwenyeji asulubike’ . 
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali inawapa matumaini makubwa wakulima wa Tanzania , kwa mipango kabambe ya kilimo cha kisasa, pamoja na uwekezaji mkubwa wa kilimo utakaogharimu mabilioni za dola la kimarekani kutoka kwa wanaoitwa wafadhili, hoja za msingi ni kama kilimo hicho kina malengo ya kumnuufaisha mkulima wa Tanzania , au malengo yake ni kupokonya ardhi ya wazawa na kisha kuwageuza vibarua /manamba ndani ya ardhi yao!

Mheshimiwa Spika,
Utafiti uliofanya na HakiArdhi juu ya hali ya maeneo yaliyokuwa ya Nafco, NARCO na Mashamba yaliyotelekezwa wamebainisha yafuatayo:

1) Ubinafsishwaji wa mashamba ulitawaliwa na utata na udanganyifu mkubwa hali iliyopelekea uadui baina ya wawekezaji na wakulima wadogo wadogo kwa upande mmoja na mgogoro kati ya wakulima wadogo na wafugaji kwa upande mwingine 

2) Katika maeneo ya yaliyokuwa mashamba ya Ngano, Hanang (Hanang Wheat Complex (HWC)) na Dakawa Ranch iligundulika kwamba wakati wananchi wanaozunguka mashamba hayo wana mahitaji makubwa sana ya ardhi wawekezaji na vigogo wenye fedha wamejilimbikizia maeneo makubwa ambayo hawayaendelezi kwa kwa ukamilifu
[1]

Kambi ya upinzani inaitaka serikali ilieleze Bunge hili tukufu na watanzania kwa ujumla nini kilichojiri katika ugawaji wa ardhi ya iliyokuwa Dakawa Ranch na ni wanakijiji wangapi walinufaika na mgao huo!

3) Wawekezaji kuwakodisha wananchi wenyeji mashamba kwa ajili ya kilimo na kuwatoza fedha. Haya yalitokea katika Mashamba yanayomilikiwa na Rai Group ambapo wananchi walikuwa wanakodisha $ 10 kwa ekari. Hali kama hii pia inafanyika katika Shamba la mpunga Mbarali na Kapunga, yote yakiwa wilaya ya Mbarali.[2]
4) Mashamba yaliyotakiwa kurejeshwa kwa wananchi lakini hayajarejeshwa , kati ya mashamba hayo ni shamba la Gawal na Warret ,lililopo Hanang lenye ukubwa wa hekta 4,000. Maamuzi ya kuyarejesha mashamba kwa wananchi yalifanyika toka mwaka 2004/05.[3] Kambi ya upinzani inataka kauli ya serikali kuhusiana na mustakabali wa mashamba haya! Kambi ya upinzani inaitaka pia serikali itoe tamko juu ya mustakabali wa shamba la Bassotu.

KIJIJI CHA CHASIMBA- BOKO – DSM
Mheshimiwa Spika,Hivi karibuni kumekuwa na matamko mbali kutoka kwa kampuni ya Saruji, (Tanzania Portland Cement Co. Ltd), ikitishia kufunga kiwanda, kwa madai kwamba hawana eneo la kutosha . Hoja yao kubwa ni kwamba wananchi wa kijiji cha Chasimba wamevamia eneo lao! Na kwamba wanashindwa kujipanua kama kiwanda.

Mheshimiwa Spika,Nimeona nilizungumze hili ili kuondoa upotoshwaji unaotaka kufanywa na kiwanda husika. Ni muhimu bunge hili tukufu likafahamu kwamba , Chasimba iko ndani ya ,Kijiji cha Boko, kijiji ambacho kiliandikishwa kama kijiji kwa mujibu wa sheria ya kuandikisha vijiji,kutambuliwa kwa Vijiji vya Ujamaa na Uongozi wa Vijiji ,1975 na hati kutolewa 25/2/1976[4]. Na hakuna mazingira yoyote yanayoonyesha kwamba kijiji hicho kilifutwa ama kubatilishwa.Lakini kama ilivyo kawaida yetu, kuendekeza wawekezaji dhidi ya wenyeji, wanakijiji waliuzwa wakiwa ndani ya ardhi yao, ndipo likaja suala la kujalidiana kuhusu fidia! Zoezi ambazo liliendeshwa kihuni hasa ikizingatiwa kwamba mwekezaji alikuwa na hati tayari! 

Mheshimiwa Spika,Wakati mwekezaji akidai anamiliki eneo lote la viwanja 1,4 na 7 kuna nyaraka za Serikali zinazoonyesha kwamba mwekezaji husika hakupewa umiliki wa eneo lote, kuna eneo ambalo lilibaki serikalini na mchakato wa kutengeneza hati mbili ulikuwa umefanyika na kufikia hatua za mwisho kabisa na nyaraka zipo!

Mheshimiwa Spika,Hoja ya kiwanda kushindwa kujitanua kwa sababu haina eneo la kutosha ,hazina mashiko hata kidogo. Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni ya tarehe 30/5/2002 kwenda kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya makazi, Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makazi. Barua husika inaelezea ombi ambalo manispaa ya Kinondoni ililipata kutoka kwa M/S Tanzania Portland cement company Ltd la kutaka kugawanywa kiwanja na 1,4 & 7.

Mheshimiwa Spika, barua husika inabainisha kwamba kikao cha kamati ya Mipangomiji na Mazingira kilichofanyika 22/5/2002 kililijadili suala hilo na kulikubali kutokana na wawekezaji katika kiwanda hicho kutokuwa tayari kulipia eneo ambalo si la uzalishaji na wala si la malighafi! Kwa ujumla eneo lote lina ukubwa wa hekta 922.22, eneo linalohusika na uzalishaji na malighafi lina ukubwa wa hekta 685. Eneo ambalo halitumiki na mwekezaji ni hekta236.63. Ni eneo hili ambalo ndilo lina makazi ya wananchi ,ambao wengi wao walidhulumiwa kwa kulazimishwa kumpisha mwekezaji! pasipo utaratibu wa kisheria kufuatwa!

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunaishauri Serikali, ambayo inataka kuwaondoa wananchi kwa nguvu, kuliangalia hili suala kwa busara ya hali ya juu. Tofauti na maeneo mengine ambayo kuna uvamizi wa maeneo ya watu, wananchi eneo hili, wengi wao ni watu wazima, ambao wana kila ushahidi wa kuonyesha kwamba pale ni asili yao na kilichofanyika ni dhuluma dhidi yao kupisha wenye fedha. Na hawako tayari kuacha makazi yao, wakiungwa mkono na Mbunge wao na madiwani wao wa Kata za Wazo na Bunju (CCM)! Tumeweka itikadi pembeni!
 UFISADI WA ARDHI NA MUSTAKABALI WA MTANZANIA MASIKINI

MKOA WA MBEYA
Mheshimiwa Spika, katika wilaya ya Mbarali, shamba la Mpunga la Mbarali (Mbarali Rice Farm- ekari 14437) na shamba la mpunga la Kapunga (ukubwa ekari 18425) yalikuwa ndio chanzo cha mapato cha wananchi wa eneo husika. Mashamba haya yalikuwa yanahudumia watu zaid ya 30,000 na vijiji kumi . Ardhi hiyo pia ilikuwa inahudumia watu wa Iringa na wilaya nyingine za Mbeya. Mipango ya awali ya Serikali , mwaka 2003/2004 kama ilivyobainishwa na na aliyekuwa Waziri wa Kilimo ilikuwa ni kuyabinafsisha mashamba hayo kwa wakulima wadogo wadogo, mpango ambao ungejumuisha mashamba ya Ruvu na Dakawa.

Mheshimiwa Spika,Kutokana na nguvu ya mafisadi kuizidi hekma ya serikali , na licha ya kilio cha aliyekuwa mbunge wa Mbarali kipindi hicho , Mhe . Esterina Kilasi , serikali iliamua kuuza eneo husika kwa kampuni ya Highland estates Ltd . Mmiliki wa sasa Bwana Nawab Mulla ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya. Wananchi wamegeuka wapangaji kwa kukodisha maeneo ili waweze kulima na kujipatia kipato! 

Mheshimiwa Spika, 
wakati Shamba la Mbarali akipewa kwa bei ya kutupa Mwenyekiti wa CCM, shamba la kapunga[5] lilibinafsishwa na kukabidhiwa kwa kampuni ya Export Co. Ltd kwa bei ya kutupa ya shilingi bilioni 2.3, mmiliki akiwa bwana JEETU Patel ( Jina halisi Jayantkumar Chandubhai Patel). 

Mheshimiwa Spika, 
hii ndio Tanzania ambayo, wazawa wananyang’anywa ardhi, maeneo yote muhimu na yakimkakati na kukabidhiwa wageni, au watu wenye mamlaka na fedha, huku ikiwaacha wazawa kubaki vibarua au wakulima wadogo wanaotegemea hisani ya mabeberu!

Mheshimiwa Spika, 
bado mustakabali wa shamba la mahindi Mbozi haujajulikana, serikali inataka kumpa mwekezaji, wakati wananchi wana uhaba wa ardhi kwa matumizi yao! Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe majibu kuhusiana na hatma ya shamba la mahindi mbozi. Halikadhalika, Kambi ya Upinzani inaitaka serikali iliambie Bunge hili tukufu, ni vigezo gani vilivyotumika kupata wanunuzi wa shamba la Mpunga la Mbarali , shamba la Kapunga, na mashamba husika yaligawiwa kwa maslahi ya nani?

MKOA WA MARA
Mheshimiwa Spika, Musoma mjini kumekuwa na mtafaruku mkubwa kati Jeshi la wananchi JWTZ na wananchi wa Bukanga na Buhare (Mgaranjabo) kutokana na jeshi kujimilikisha maeneo yao ya asili, waliyokuwa wakitumia kwa ajili ya matambiko kwa Kabila ya Wakwaya. Hivi sasa wananchi hao hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo, jambo hilo limezusha chuki kubwa sana kati ya Jeshi na jamii ya Wakwaya wakazi wa Musoma Mjini.

MKOA WA MOROGORO
Mheshimiwa Spika,Matatizo ya ardhi,kwa wakubwa kunyang’anya wanyonge ardhi imeikumba pia Halmashauri ya wilaya ya Mvomero. Mgogoro huu unahusu shamba namba 299 (iliyokuwa NARCO Ranches),lenye ukubwa wa hekta 49,981. 

Mheshimiwa Spika,
 katika shamba hili, taarifa zinaonyesha kwamba 30,007 hektas walipewa Mtibwa sugar licha ya malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba eneo walilopewa ni kubwa sana. Taarifa za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba, maeneo ambayo yalikuwa yamepangwa kugawiwa wanakijiji, wa kijiji cha Wami, yamegawiwa ’wananchi’ wafuatao: 

1) Bwana Philip Mangula, aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, ndio anaongoza kwa kuwa ’mwanakijiji’ mwenye eneo kubwa, alipewa hekta 2000. 
2) Bwana John Malecela, Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM alipewa hekta 100,
3) Jenerali mstaafu Ngwilizi, ambaye pia alikuwa waziri wa serikali za mitaa awamu ya tatu alipewa hekta 100 kati ya hekta 5000, zilizosemwa wamepewa wakulima wadogowadogo wa kijiji.
4) Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, anamiliki hekta 2000, ambazo hazijaendelezwa, 
5) Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Frederick Sumaye hekta 500 na 
6) Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, hekta 1000 (ila tofauti na wengine shamba hili limeendelezwa).

Mheshimiwa Spika, Kambi ya upinzani inahoji, kama hawa watajwa hapo juu ni wakazi wa kijiji cha Wami- Dakawa? Na ni vigezo gani vilitumika kuwanyima ardhi wanakijiji na kuwapa wakubwa hawa? Serikali haioni kwamba mgao huu wa ardhi uliojaaa dhuluma na upendeleo unahatarisha maisha ya watanzania na usalama wa nchi kwa ujumla? 

Mheshimiwa Spika
, Wananchi wa maeneo haya wana hasira na serikali yao kwa kuwa wameshaambiwa hakuna tena eneo la kugawa, wakati walitozwa shilingi 20,000 kila mmoja kwa madai kwamba wangepewa hekta 5. Ahadi ya hekta 10019 kwa wakulima na wafugaji, imegeuka hewa! Tunakwenda wapi kama nchi? Mheshimiwa Spika Kambi ya upinzani , inaitaka serikali kuangalia upya zoezi la ugawaji wa ardhi katika maeneo yote yenye utata! Ambayo yalitawaliwa na rushwa,ubabe na udanganyifu.

MKOA WA PWANI -SIMBA MOTORS VS WAKAKIJIJI KITONGOJI CHA UNDINDIVU, MAPINGA – BAGAMOYO

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kijiji cha Mapinga, kitongoji cha Undindivu chenye idadi ya watu zaidi 1400 wamekuwa wakimiliki eneo la Undindivu kwa ajili ya kilimo na ufugaji toka mwaka 1960. Kama ilivyo kawaida yetu ,kampuni ya Simba Motors (T) Ltd ilimilikishwa eneo lote la kitongoji cha undindivu bila wananchi au serikali ya kitongoji na kijiji kujulishwa. Kampuni hiyo ilipima kwa kutumia mpimaji binafsi na ilimilikishwa shamba hilo lenye hecta 322. Baada ya kampuni husika kupima na kumilikishwa bila kufuata sheria, takriban miaka 17 imepita kampuni hiyo haijawahi kuendeleza shamba hilo,kampuni haijawahi kuliendeleza eneo hilo, si kwa kilimo au ufugaji.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa, kuna mgogoro mkubwa baina ya Simba Motors na wananchi wa kitongoji cha undindivu, na kutokana na shamba husika kumilikishwa kwa tajiri mmoja , wakati wakazi wa maeneo hayo wamekosa;1)Maeneo kwa ajili ya huduma muhimu za jamii. 2) Maeneo kwa ajili ya kupanua makazi yao ya kuishi,kwa sababu robo tatu ya eneo la kijiji limamilikiwa na tajiri huyo.

Mheshimiwa Spika,
 Kambi ya upinzani inaitaka serikali, kuutafutia mgogoro huu ufumbuzi wa kudumu. Hatuwezi kuendelea kukaa kimya , na kuacha wananchi wetu masikini wakipokonywa maeneo yao kwa faida ya matajiri wachache! Mheshimiwa waziri , Kambi ya upinzani inajua kwamba ofisi yako ilishaletewa taarifa kwa barua ya tarehe 15/12/2010,hakuna kilichofanyika mpaka sasa. Tunataka majibu!

MKOA WA RUKWA – AGRISOIL , KILIMO KWANZA NA HATMA YA TANZANIA

Mheshimiwa Spika, Nchi yetu imefika hapa ilipo, kutokana na watu wenye dhamana kuingia mikataba mibovu ambayo badala la kuisaidia nchi imekuwa ni msalaba mkubwa ! na kuwaacha watanzania katika limbwi la umasikini. Hivi karibuni kampuni ya Agri- Sol Energy LLC na Kampuni ya Serengeti advisors Ltd , inayoongozwa na Bwana Iddi Simba (aliyekuwa Waziri wa viwanda na Biashara, awamu ya tatu) na Betram Eyakuze kwa pamoja wameunda kampuni ya Agrisol Energy Tanzania , wameingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Mkataba ambao unatarajia kuipa kampuni husika miliki ya miaka 99 ya maeneo ya lugufu, Hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.
Mheshimiwa Spika, 
Masharti ya Msingi katika makubaliano baina ya Halmashauri husika na wawekezaji ni yafuatayo;
a) Kodi ya ardhi ( Land rent) ambayo ni Tshs. 200 kwa hekta
b) Ushuru wa kisheria wa Halmashauri ,
c) ada itakayolipwa halmashauri ni Tsh 500 kwa hekta.
d) Na sharti la mwisho, kama mgogoro utatokea baina ya pande zote mbili, 
busara itatumika kutatua mgogoro, ikishindikana chemba ya Biashara ya Kimataifa ( ICC) ndio atakuwa msuluhishi! 

Mheshimiwa Spika
, tunakwenda wapi? Umasikini ndio utufanye tuwe mambumbu wa kufikiri? Hivi kwa nini hatujifunzi ?

Mheshimiwa Spika,
 Katika hatua za awali,madiwani wa Halmashauri husika walikataa kutoa maeneo yote mawili,waliagiza mwekezaji apewe eneo moja na kwa kipindi cha miaka 20. Kama ataonekana kufanya vizuri,wangefikiria kumwongezea muda na eneo! Kama kawaida, walioonekana kuwa wakali wakapelekwa Marekani, kwa siku nne! Baada ya kurejea, Nchi ikaingizwa kwenye mkataba mwingine ambao utaigharimu nchi miaka mingine 99 kuweza kujinasua! 

Mheshimiwa Spika, 
Si dhamira ya kambi ya upinzani kudhihaki ama kukatisha tamaa uwekezaji , tunafahamu kwamba serikali inaichukulia Agri Sol Energy kama sehemu ya mkakati wake wa Kilimo Kwanza, lakini hawa wawekezaji ambao wanaitwa wakubwa, mashamba ambayo wanayaendesha ,haswa yale yaliyoko Marekani na yaliyotembelewa na maafisa wa serikali ,wakiongozwa na ofisi ya Waziri Mkuu yana ukubwa wa ekari 17,900, (ambapo ekari 13,195 ni za mahindi na ekari 4705 ni maharage). Na shamba hilo limeajiri watu 13, hivi hawa ni wakulima kweli? 
Mheshimiwa Spika,Itakumbukwa kwamba kulikuwa na mkakati uliokuwa ukiendeshwa kwa usiri mkubwa na kwa kasi ya hali ya juu kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI wa kuwasambaza wakimbizi wanaokadiriwa kufikia 162,000 nchi nzima, katika mikoa mbali mbali. Mchakato ambao ulipata upinzani mkubwa hapa Bungeni na kutoka mikoa husika. Huu ulikuwa ni mkakati wa makusudi ili maeneo husika yawe wazi kwa wawekezaji hao kukabidhiwa, na mbaya zaidi wakimbizi waliambiwa bayana kwamba sharti la kupewa uraia wa Tanzania ni kuondoka maeneo hayo!

Mheshimiwa Spika, 
Ni muhimu ikaeleweka kwamba, huu mtindo wa kuwageuzwa watanzania manamba ndani ya nchi yao kwa kutoa ardhi kwa wageni utakuja kusababisha machafuko hapo baadae....ieleweke hoja hapa sio kulisha taifa na kupata ziada kusafirisha nje ya nchi, hoja hapa ni kumnufaisha mtanzania katika mipango yote endelevu ya matumizi ya ardhi! Na kama ni suala la chakula na kusafirisha nje ya nchi chakula hicho kipo tatizo ni kukitoa kwa wakulima na kufikisha sokoni, ushahidi huo upo kuwa mahindi ni mengi kuliko uwezo wa wananuni (Rukwa, Songea, Iringa-Ludewa n.k.)

UKIUKWAJI WA SHERIA YA ARDHI, NO. 4 YA MWAKA 1999

Mheshimiwa Spika, 
Vifungu vya 19(2) ,20 (1), 20 (2), 20(3) na 20(4) vya Sheria ya Ardhi vinatoa masharti ya umiliki wa ardhi kwa watu ambao sio watanzania. Kwa ujumla wake vifungu husika vinapiga marufuku ardhi kupewa kwa wageni, isipokuwa tu kwa madhumuni ya uwekezaji chini ya Sheria ya uwekezaji , No. 26 ya mwaka 1997. Na ili ardhi husika iweze kupatikana lazima kwanza itambuliwe ,itangazwe kwenye gazeti la serikali na iwe ‘ allocated’ kwa Kituo Cha Uwekezaji, ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la kumpatia Mwekezaji.
Mheshimiwa Spika,
 Haya yote hayajafanyika, na kinachotaka kufanyika kwa kutumia vibaraka wa kitanzania , ni kuhakikisha kwamba wabia ‘vibaraka’ wa kitanzania wana kuwa na hisa nyingi katika umiliki wa ardhi ili kuepuka kikwazo cha kupitia katika Kituo cha uwekezaji. 

Mheshimiwa Spika, kuhusu mamlaka ya kuingia ubia (joint venture) na mwekezaji ambaye si Mtanzania kama ambavyo inaonekana ni kamchezo ambako kanataka kuchezwa na Serengeti Advisers Limited, Mabadiliko ya Sheria ya Ardhi yaliyofanyika mwaka 2004, Sheria Na. 2/2004 The Land (Amendment ) Act 2004 Kifungu 19 (1), (2) (c) kinasema ili kufanikisha masharti ya uendelezaji wa ardhi, raia wa Tanzania anayemiliki ardhi anaweza kuingia ‘joint venture’ na mwekezaji ambaye si raia wa Tanzania kwa madhumuni ya uwekezaji chini ya Sheria ya Uwekezaji , Sura ya 38.

Kwa mujibu wa Kifungu hicho ubia unafanywa na mzawa na mgeni. Kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ‘ The Tanzanian Citizenship Act’, Cap 357. 
Shirika la umma au Kampuni au halmashauri haiwezi kuwa na sifa za kuwa raia. Hivyo kwa mujibu wa kifungu 19 (2) (c) si halmashauri ya wilaya ya Mpanda wala kampuni ya Serengeti Advisers yenye uwezo wa kutoa ardhi yake kwa mtu ambaye si raia ili kuwekeza kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika
, kwa kuzingatia maelezo ya vifungu nilivyovitaja hapo juu(isipokuwa kama kuna mabadiliko ya sheria ambayo hadi sasa haifahamiki), Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kampuni ya Serengeti Advisers haina uwezo wa kuwekeza kwa pamoja ‘ joint venture ‘ na wawekezaji ambao si watanzania mpaka hapo sheria zitakapofanyiwa marekebisho.

Kambi ya upinzani inaitaka Serikali ituambie, ilitumia utaratibu gani wa kisheria kuingia Mkataba huo wa kifedhuli na usio na maslahi hata kidogo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Taifa kwa ujumla? Nani aliwatuma? 


MIGOGORO YA ARDHI BAINA YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Mheshimiwa Spika, Kilimo na ufugaji ni ya sekta zinazoongoza kwa kutoa mchango mkubwa sana katika pato la Taifa, halikadhalika ndizo zinazoongoza kwa kutoa ajira kwani zaidi ya 80% ya Watanzania wamejiajiri katika sekta hii,haswa vijijini. Hivyo basi kuboresha hizi sekta mbili, maana yake ni kwamba tutakuwa tumeboresha 80 % ya maisha ya watanzania, kwa kuwa na uhakika wa kipato, usalama wa chakula na kuongezeka kwa pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika,
 Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu kutokea kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji, chanzo cha migogoro hiyo ni kutokana na kutokuwa na mipango thabiti ya serikali ili kubainisha /kutenganisha maeneo maalum kwa ajili ya wakulima , halikadhalika wafugaji.

Mheshimiwa Spika, 
Sheria yetu ya ardhi , No. 4 na No. 5 ya mwaka 1999 imeainisha utaratibu ambao miliki ya ardhi ya mtu mmoja mmoja ama kikundi inavyotambulika kisheria mijini na vijijini kisheria ama kimila. Hata hivyo utaratibu wa utwaaji na umiliki ardhi hasa vijijini kwa matumizi ya wafugaji , wachungaji na wawindaji haujaainishwa ipasavyo !Mikakati ya kutenga ardhi hasa ya wafugaji imekuwa finyu mno kiasi kwamba wakulima na wawekezaji wameendelea kuhodhi/kuvamia ardhi ya wafugaji kwa msaada wa mawakala wa serikali.[6] Na wakati mwingine wafugaji wamekuwa wakivamia maeneo ya wakulima kutokana na kukosa maeneo mwafaka kwa ajili ya malisho.
Mheshimiwa Spika,Tafiti pia zimeonyesha kwamba ardhi ya wafugaji imekuwa ikichukuliwa kwa ajili ya matumizi ya wawekezaji , kugeuzwa kuwa hifadhi za taifa au game reserves! Matokeo yake wafugaji wanageuka watu wa kutangatanga! Wakati serikali imekuwa ikiwataka wafugaji waondokane na njia za kizamani za kufuga, bado haijaonyesha njia mbadala za ufugaji wa kisasa!



Mheshimiwa Spika, Kambi ya upinzani inaitaka serikali , itueleze ina mikakati gani katika kuhakikisha kwamba maeneo rasmi ya wafugaji yanabainishwa ili kuepusha umwagaji damu na migogoro isiyo na tiba huko mbeleni.

Halikadhalika, kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe tamko juu ya tatizo la mpaka na mgogoro wa wakulima na wafugaji wa jamii ya Wamasai katika eneo la 
vijiji vya Izava (Chamwino) na Chitego (Kongwa).  Mgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ulisababishwa na maamuzi ya kibabe yaliyofanywa na wakuu wa wilaya hizi mbili (mwaka 2006) , wakishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri kipindi hicho!
Mheshimiwa Spika, Wakulima wa maeno haya wanalalamikia wafugaji ambao waliingizwa kibabe katika maeneo yao, bila kuwashirikisha kwa nguvu za ’kigogo mmoja’, matokeo yake mashamba yao ndio yamegeuka malisho ya mifugo hiyo! Kumekuwa na tuhuma ya ushiriki wa skari wa Kongwa katika zoezi hili kandamizi! Kambi ya upinzani inaitaka Serikali ifuatilie mgogoro huu ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea, hasa ikizingatiwa kwamba matukio ya kushambuliana ,kujeruhi na kutishia maisha imekuwa ni jambo la kawaida baina ya pande mbili.

MATATIZO YA TATHMINI NA MALIPO YA FIDIA

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi kulalamika kupunjwa ama kutokulipwa kabisa fidia pale ambapo wanatakiwa na serikali kuhama maeneo yao ili kupisha matumizi mapya ya ardhi. Mheshimiwa Spika sheria zetu zinatamka bayana kwamba, pale ambapo mwananchi anapochukuliwa eneo lake na serikali kwa mamtumizi mengine na hivyo kutakiwa kuhama anatakiwa kulipwa fidia inayojumuisha, thamani ya ardhi, usumbufu, usafiri na hasara ambayo muathirika ataipata kutokana na kuchukuliwa eneo lake. 

Mheshimiwa Spika, 
hata hivyo kumekuwa na malalamiko kila pahala ambapo wananchi wanatakiwa wasimamishe shughuli zao kupisha matumizi mapya ya ardhi. Serikali hailipi fidia ya kutosha na hata wananchi wakilalamika serikali inaendelea miradi. Badala ya fidia kumwacha mwananchi awe katika hali aliyokuwa mwanzo,mfumo wa fidia wa nchi yetu ,haswa maeneo yanapochukuliwa na serikali (ambayo ndio hiyo hiyo inafanya tathmini na kuamua kiasi gani kilipwe) unamwacha mwathirika fukara zaidi! 

a) Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe maelezo juu ya hatma ya wananchi wa Kurasini Mabwawani ambao tangu nyumba zao zifanyiwe tathmini miaka miwili iliyopita ili kupisha upanuzi wa bandari, kumekuwa na kimya kingi na wakiuliza kuhusu hatma yao, hawajibiwi kitu!kuna kundi ambalo limelipwa, kuna kundi lingine halielewe nini kinachoendelea na wanashindwa kuendeleza maeneo yao


b) Kambi ya upinzani inaitaka wizara ya ardhi itoe maelezo juu ya hatma ya wananchi wa kijiji cha Mabwepande, kata ya Mabwepande Jimbo la Kawe ambao miaka minne iliyopita serikali ilikwenda kufanya tahmini na kuwaagiza wananchi kutokufanya maendeleo yoyote ili kupisha upanuzi wa chuo cha IFM. Hakuna kilichofanyika mpaka sasa, wananchi waliokuwa wanategemea kilimo, wamezidi kufukarishwa, serikali ikiulizwa haina majibu. Matokeo yake maeneo ambayo waliambiwa wayaache sasa yamevamiwa na genge la wavamizi, si wizara, halmashauri ya manispaa ya kinondoni ama vyombo vya usalama vinavyochukua hatua licha ya kupewa taarifa ya uvamizi huu!


c) Kambi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya wananchi wa Kigamboni (ambao wengi walikuwa wanafanya kazi za kilimo) ambao wanalalamikia zoezi la kuchukua maeneo yao kupisha ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni kutawaliwa na rushwa, maeneo kuthaminishwa bei ndogo, wakati huo huo serikali baada ya kulipa fidia kiduchu wanauza maeneo husika kwa bei ya kutupwa,bei ambayo mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu!



d) Kambi ya upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya wananchi wapatao 1600 wa wilaya ya Mbarali waliotakiwa waondoke maeneo yao ili kupisha upanuzi mbuga ya Taifa ya Ruaha? Serikali ilitoa shilingi bilioni 6.5 tu kwa wakazi wote. Kwa tathmini ya kawaida kila mwananchi alipewa shilingi milioni 4.5. Hivi kwa maisha ya sasa kuna nyumba inayoweza kujengwa na kukamilika kwa kiasi hicho cha fedha? Huu ni unyonyaji na udhalimu ulio dhahiri.

e) Kambi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya fidia ya wananchi wa Jimbo la Ubungo Kata ya Kwembe wanaopaswa kuhama kupitisha ujenzi wa majengo wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Afya (MUHAS) Mloganzila. Wakati wa kuhitimishwa kwa bajeti ya Waziri Mkuu katika mkutano huu wa bunge serikali ilieza kwamba tathmini ya fidia inaendelea na kwamba wapo wananchi ambao tayari wamelipwa fidia na wengine bado hawajalipwa mpaka sasa. Kambi ya Upinzani inaitaka serikali kuzingatia kwamba fidia iliyolipwa kwa wananchi wachache ni ya mali na mazao; hata hivyo wananchi hawajalipwa fidia ya ardhi. Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa maelekezo kwa wizara zinazohusika kuhakikisha fidia stahiki inalipwa. Mwaka 2010 Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ilifanya mkutano na wananchi na kuwaahidi kulipa fidia ya ardhi kwa mujibu wa sheria; kambi ya upinzani inataka serikali ieleze malipo hayo yatatoka kwenye fungu lipi na yatalipwa lini?

MALALAMIKO DHIDI YA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU (CDA)

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2004 , Serikali kupitia wakala wa majengo mkoani Dodoma, waliwauzia wananchi, nyumba zilizokuwa zinamilikiwa na lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC). Malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi hawa wa Tambukareli,ni kunyimwa hati za nyumba zao na CDA ilhali wameshalipia nyumba hizo kwa ukamilifu. Sababu zinazotolewa na CDA, zisizo na mashiko ni kwamba eti Serikali ilitoa uamuzi wa kuuza nyumba bila kuwahusisha CDA , hivyo hawatambui uuzwaji wa nyumba hizo!

Mheshimiwa Spika,
Kambi ya upinzani inaitaka serikali kutoa maelekezo kwa CDA kutoa hati husika, ni suala la kibri na jeuri kwa taasisi ya serikali kuhoji maamuzi ya serikali, au leo tuelezwe kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano inafanya kazi chini ya CDA? Kama kulikuwa na uzembe ndani ya Serikali kwa nini Wananchi hawa masikini waliodunduliza vihela vyao wapate makazi waumizwe? Kambi ya upinzani inataka kauli thabiti ya serikali kuhusiana na hili!

SHERIA NA. 5 YA ARDHI YA VIJIJI NA MUSTAKABALI WA TAIFA

Mheshimiwa Spika,Sheria ya Ardhi ya Kijiji inatoa mamlaka kwa Halmashauri ya kijiji kusimamia ardhi yote ya kijiji. Halikadhalika Halmashauri ya kijiji imepewa mamlaka ya kugawa ardhi baada ya kuruhusiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji. Uzoefu umeonyesha kwamba kutokana na kutokuwa na ufahamu mpana wa sheria, watu wenye fedha wamekuwa wakitumia fursa hii ya kisheria vibaya kwa kuwarubuni viongozi wa vijiji, na hatimaye kugawa maeneo ya kijiji kwa wageni wenye fedha wachache, huku ikiwaacha wanakijiji bila ardhi yoyote. 

Mheshimiwa Spika,
Hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo watu ambao sio watanzania wanatumia upenyo huu wa kisheria, na kumilikishwa maeneo makubwa ya kijiji kinyemela! Kambi ya upinzani imepata malalamiko kutoka kwa wanakijiji wa kijiji cha Orngadida, Kata ya Qash, Babati ( taarifa ambayo Waziri wa Ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji –Halmashauri wanayo). Wanakijiji hao wanawatuhumu viongozi wa serikali ya kijiji wakishirikiana na diwani kuuza Ardhi kwa wageni pasipo kuwashirikisha, wanakijiji wamemwandikia Mkuu wa wilaya ya Babati barua mbili ambazo nazo hazijajibiwa! 

Mheshimiwa Spika,
 Hakuna ubishi kwamba kuna wageni wengi waliopata maeneo ya vijiji kinyemela kwa kutumia upenyo huo, wakati sheria ya Ardhi No.4 , kifungu na 20 kinakataza wageni kumiliki ardhi nchini isipokuwa kwa malengo ya uwekezaji tu, na ambao umiliki wake lazima upitie Kituo cha uwekezaji Tanzania , na si vinginevyo. 

Mheshimiwa Spika,
 Kambi ya upinzani inaitaka serikali iliambie Bunge lako tukufu,ni lini imefanya tathmini katika vijiji vyetu ili kuweza kubainisha ardhi zilizotolewa na Halmashauri za kijiji na uhalali wake. Ni maoni ya Kambi ya upinzani kwamba sheria hii isipoangaliwa kwa umakini itasababisha umwagaji damu mkubwa hasa pale wananchi watakapohisi kunyang’anywa ardhi yao kifisadi au vinginevyo. Na mbaya zaidi Mheshimiwa Spika,zoezi hili linafanywa hata mijini, na serikali za mitaa ambazo hazina mamlaka ya kugawa ardhi. Mchezo ambao wanafanya kwa kushirikiana na watendaji wa manispaa, na baadhi ya maafisa wa Wizara!
UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI MKOA WA DAR ES SALAAM
Mheshimiwa Spika; kutokana na malalamiko ya wananchi mbalimbali kuhusu uvamimizi wa maeneo ya wazi ya umma katika mkoa wa Dar es salaam, Serikali iliunda kamati ya kufanya uchunguzi kuhusu uvamizi katika maeneo husika. Kamati ilikamilisha kazi yake tarehe 13 Julai 2010. Pamoja na majibu ya Waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi aliyoyatoa tarehe 1 Julai 2011 wakati akijibu maswali bungeni kuhusu hatua ambazo serikali imechukua toka mamlaka husika zilipokabidhiwa ripoti husika; kambi ya upinzani inataka maelezo zaidi kutoka kwa serikali kwa kuwa mwaka mmoja umepita toka uchunguzi huo ufanyike na sehemu kubwa ya viwanja bado vipo mikononi mwa wavamizi.

Mheshimiwa Spika;
 kambi ya upinzani inaitaka serikali ieleze: Ni viwanja vingapi vimerudishwa na vingapi bado vipo mikononi mwa wavamizi? Ni lini serikali itarejesha viwanja vyote vilivyobaki kwenye matumizi yake kwa mujibu wa sheria kwa kurejea mapendekezo ya kamati? Ni hatua gani zimechukuliwa kwa wahusika Wizarani na kwenye halmashauri walioshiriki kusababisha hali hiyo ukiondoa maafisa wachache ambao wamefikishwa mahakamani kutokana na kesi ya kiwanja kimoja hivi karibuni? Kwa kuwa sasa Wizara ina kada ya askari (land rangers) ni lini askari hao watatembelea maeneo yote yaliyotajwa kuvamiwa kwa mujibu wa taarifa ya kamati ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa?
Mheshimiwa Spika; athari za uvamizi wa viwanja vya wazi ni kubwa katika mipango miji na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Mathalani katika Manispaa ya Kinondoni kwenye kiwanja na. 856 Msasani beach ambacho kwa mujibu wa Ramani ya upimaji iliyosajiliwa namba 29331 ilikuwa ni kwa matumzi ya wazi, lakini baadae kilimilikishwa kwa mtu binafsi. Athari yake ni kuzibwa kwa njia ya mkondo kuelekea baharini yamezibwa na hivyo kuleta mafuriko katika barabara na makazi ya watu wa eneo husika; hali hiyo ipo pia katika majengo ya May Fair na Markham. Kambi ya Upinzani inataka Serikali ieleze hatua zipi itachukua ili kuepusha wananchi wa maeneo ya Msasani, Mikocheni na maeneo mengine katika jiji la Dar es salaam yaliyojengwa majengo kinyume cha sheria na mipango miji na hivyo kuleta athari kubwa kwa maisha ya wananchi.

SEKTA YA NYUMBA


Mheshimiwa Spika,
 sekta hii ni sekta pekee inayoweza kuleta na kutekelezwa kwa dhana nzima ya maisha bora kwa kila mtanzania. Nchi yetu na watanzania kwa ujumla bado tuna matatizo makubwa ya nyumba bora na za bei nafuu kutokana na bei kubwa ya cement na bati bidhaa muhimu katika kutimiza azma ya ujenzi.
Mheshimiwa Spika, tulisema na tunasema kuwa bei ya simenti na bati inaweza kuwa chini ya shilingi elfu saba, kama serikali itakuwa na utashi wa kuwahudumia wananchi kwa dhati, Wakati ukinunua simenti Uturuki, na Paksitani ukinunua tani 600,000 bei ya tani moja ni dola za Marekani 70 hadi bandarini. Guangzhou –China tani moja ni dola za marekani 26. Kwa hesabu za kawaida kwa mfuko mmoja ni dola 3.5 sawa na shilingi 5,250 kama ukinunua Pakstani au Uturuki, Ukinunua China bei itakuwa dola 1.3. 

Mheshimiwa Spika
, Kambi bado inasisitiza kuwa kama Serikali inadhamira ya kweli mfuko wa simenti hauwezi kuuzwa zaidi ya shilingi 7,500. Hivyo basi tunaitaka Serikali itueleze kwanini bei ya simenti inauzwa zaidi ya shilingi 14000 kwa Dar es salaam na kwa nje ya Dar es Salaam bei ni zaidi ya hapo, wakati malighafi zinapatikana hapa hapa nchini na kiwanda kikubwa cha simenti kinatumia gesi asili ili kupunguza gharama za umeme. 

Mheshimiwa Spika,
 Serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama hizi na ni faida kiasi katika kodi tunayopata kwa kuwalangua watanzania. Serikali haioni kwamba ina wajibu wa kuondoa hizi kero wananchi wajenge nyumba bora na kwa bei nafuu?

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA-(NHC)

Mheshimiwa Spika,
Shirika la Nyumba la Taifa, lilipoanzishwa mwaka 1962 , moja kati malengo yake ilikuwa ni kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya watanzania wafanyao kazi mijini . Hata hivyo kwa kadiri siku zilivyosonga mbele, shirika hili liligeuka kutoka kuwahudumia masikini na watu wenye kipato cha kati na badala yake kuwahudumia watu wa kipato cha juu. 

Mheshimiwa Spika
, Shirika la Nyumba la Taifa linahudumia asilimia 0.5 tu ya watanzania wote wa nchi hii, swali la msingi ni je Serikali imeweka mikakati gani ya kuhakikisha kuwa shirika hili linahudumia watanzania wengi zaidi kwa kuwapatia nyumba za bei nafuu.

Mheshimiwa Spika,
Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, mwezi Juni 2010, Katibu Mkuu wa wizara ya ardhi, akikerwa na hali ilivyokuwa katika Shirika la Nyumba, alisema kwa sasa NHC ndilo shirika la umma linaloongozwa kwa rushwa nchini Tanzania, na kwamba baadhi ya watumishi waandamizi wameligeuza shirika hilo kuwa ni ng’ombe wao wa kukamua fedha chafu!.[7] Katibu Mkuu alikwenda mbele zaidi, kwa kutolea mfano wa nyumba iitwayo Victoria house iliyopo kando ya Barabara ya Ali hassan Mwinyi ambayo pesa ya pango ilikuwa ikiingia kwenye akaunti ya mtumishi wa shirika.

Mheshimiwa Spika, 
kumekuwa na malalamiko pia ya kutokuwa na uaminifu baina ya wapangaji, wakishirikiana na washirika wao walioko kwenye utumishi wa shirika, kulikopelekea shirika kupata hasara ya mabilioni ya shilingi kwa kuingia mikataba tata! Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa hizi, mikataba tata imekuwa ikifanyika huku ikiwashirikisha wapangaji wa asili ya kihindi kwa kiasi kikubwa ambao wanatuhumiwa kuligeuza shirika hilo kama mali yao binafsi. 

Mheshimiwa Spika, 
mwaka mmoja ukiwa umepita tangu kauli hii nzito toka kwa mtendaji wa ngazi ya juu wa wizara,Kambi ya Upinzani inaitaka serikali ilieleze Bunge hili tukufu , ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya watumishi hawa , na ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya wapangaji wasio waaminifu!


SERIKALI NA TAASISI ZAKE KUTOLIPA KODI ZA PANGO KWA WAKATI


Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi cha julai 2011 shirika lilikusanya kodi za pango pamoja na malimbikizo kiasi cha shilingi bilioni 31.

Pamoja na na jitihada za kukusanya kodi na malimbikizo na hasa yale yanayodaiwa serikali na taasisi zake, malimbikizo bado ni makubwa . Hadi machi 2011, serikali na taasisi zake ilikuwa ikidaiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.543, baada ya kupunguza malimbikizo kwa kiasi cha shilingi milioni 115, sawa na asilimia 8 tu!Kambi ya 
upinzani inataka serikali ieleze ni kwa nini imekuwa ni mdaiwa sugu, na kwa nini hailipi madeni ya shirika la nyumba?
MIKOPO YA UNUNUZI NA UJENZI WA NYUMBA

Mheshimiwa Spika,
 Pamoja na kuwepo kwa sheria ya Mikopo ya nyumba (mortgage financing act) ya mwaka 2008 na sheria ya umiliki wa sehemu ya majengo ( unit titles act) ya mwaka 2008, masharti ya mikopo hii bado ni magumu. Mfano, kwa sasa benki zanazotoa mikopo ya nyumba masharti yake ni pamoja na muda wa marejesho ya kati ya miaka 6 mpaka 15 na riba kati ya asilimia 17 mpaka 22 kwa mwaka . 

Mheshimiwa Spika, Iwapo hali hii haitabadilika , itakuwa vigumu kwa wananchi, halikadhalika shirika letu la nyumba kujenga nyumba za gharama nafuu na kwa wananchi walio wengi kuweza kumudu mikopo ya ununuzi wa nyumba. 

Kambi ya upinzani, inaitaka Serikali itueleze ni kwa namna gani imejipanga kuweza kutatua tatizo hili ! Lazima Serikali iweke Mazingira ya kuziwezesha Benki kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wawekezaji na wanunuzi wa nyumba.!!!!

KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) NA ONGEZEKO LA MTAJI (CAPITAL GAIN TAX) KWENYE MAUZO YA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SHIRIKA

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa inyowakabili watanzania wengi ni kuweza kupata nyumba za bei nafuu. Kwa sheria zetu za kodi, nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya kuuzwa inapaswa kutozwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pale inapouzwa, na anayelipa kodi hiyo ni mnunuzi!
Mheshimiwa Spika, suala la msingi ni kuwa nyumba hiyo wakati inajengwa vifaa vyote vya ujenzi ulipiwa kodi hiyo, hivyo kitendo cha mnunuzi kulipa kodi ya VAT wakati wa kununua nyumba hiyo ni kulipia kodi mara mbili (DOUBLE TAXATION). Je, serikali haioni kama haimsaidii mwananchi kuweza kuishi kwenye nyumba nzuri na kwa gharama iliyonafuu?
Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kuangalia upya mkakati wake wa kuwanyang’anya watanzania hata kile kidogo walichonacho badala ya kuwaongezea umasikini iwe ni kuwapa maisha bora kama kauli mbiu yenu inavyosema. Mfano dhahiri, kwa mwaka wa fedha 2010/11 shirika lilitarajia kujenga nyumba 49 , zenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 4.08. Kwa gharama iliyotumika, wastani wa nyumba moja ililigharimu shirika shilingi milioni 83.4.

Mheshimiwa Spika, 
kwa mujibu wa Taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Shirika la Nyumba la Taifa kuanzia Julai 2010 hadi Mei 2011 wanatarajia kupata shilingi bilioni 6.3 kutokana na mauzo ya nyumba hizo , yaani faida ya shilingi bilioni1.9 Kwa tafsiri nyingine nyumba moja itauzwa na shirika la nyumba kwa shilingi milioni 129.2, wakati gharama halisi za ujenzi ni shilingi milioni 83. Kwa kila nyumba iliyounzwa shirika limepata faida ya shilingi milioni 46.

MUSTAKABALI WA NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA


Mheshimiwa Spika,
 Hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusiana na nyumba za shirika. Wapangaji (hususan katika maeneo ya katikati ya miji) wamekuwa wakilitaka shirika liwauzie nyumba. Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe kauli, nini msimamo wake kuhusiana na suala hili,[8] lakini sisi tunaona kuwa hakuna haja yeyote ya shirika hili kuuza nyumba hizo na badala yake iweke mkazo katika kujenga nyumba ambazo zitapangishwa kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Spika, 
Sheria ya mikopo yaani "Government Loans, Guarantees and Grants Act 1974 and amendments 2003" inalifanya shirika la nyumba la taifa kulazimika kupata kibali kutoka Wizara ya Fedha hata pale ambapo halihitaji kupata dhamana ya serikali na pia hata kwa mikopo ya ndani ya nchi. Wote tunafahamu rasilimali ambazo shirika hili linazo. Pamoja na kufahamu yote, bado tumeamua kuliweka shirika hili katika urasimu mkubwa wa kiserikali wa kupata vibali kutoka wizara ya fedha bila ya sababu za lazima. Je, serikali imedhamiria ya kutekeleza ahadi zake katika ujenzi wa nyumba na kuliwezesha shirika kujiendesha kibiashara kama sheria yake inavyolitaka? Kambi ya Upinzani inaitaka serikali itoe ufafanuzi ni lini inatarajia kuanzisha mchakato wa kurekebisha sheria hiyo?



MPANGO WA UENDELEZAJI ENEO LA KIGAMBONI
Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2007, Wizara ilianza hatua za awali za kuendeleza mji mpya wa Kigamboni. Mradi huu unahusisha hekta 6500 linaloshirikisha kata 5 za Kigamboni, Tungi,Mjimwema,Vijibweni, Kibada na mitaa miwili ya Mbwamaji na Kizani kwenye Kata ya Somangila.

Mheshimiwa Spika, 
Miaka minne imepita,Kambi ya upinzani inaitaka serikali ibainishe ni lini hasa mradi huu utaanza, na michakato ya fidia kwa wananchi imefikia wapi,na ni utaratibu upi unaotumika kulipa fidia husika. Halikadhalika Kambi ya upinzani inaitaka serikali kuhakikisha kwamba kunakuwepo kwa utaratibu ulio wa uwazi, pasi na upendeleo kuhakikisha kwamba wananchi waishio ndani ya eneo la mpango ( yaani wakazi wa kata zote tano) wanabaki kwenye eneo hilo, kama ambavyo madhumuni ya mpango unavyoainisha. 

Mheshimiwa Spika,
Kambi ya upinzani ina taarifa juu ya mchakato unaofanyika baina ya serikali na shirika la nyumba la taifa unaohusiana na uendelezaji wa eneo la Tanganyika Pakers-Kawe, kama ilivyobainishwa na naibu waziri wa viwanda na biashara, wakati akijibu swali namba 246, ambapo pamoja na mambo mengine alikiri kwamba katika eneo la kawe kuna heka 180, ambalo ni eneo la makazi na ambalo halikuuzwa na Serikali kwa mwekezaji.Kambi ya upinzani inaitaka serikali ifahamu kwamba , eneo husika bado lina wakazi ambao walikuwa ni wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanganyika Pakers, na hatua zozote za kuliendeleza eneo husika,lazima uhakikishe unawahusisha kikamilifu wananchi hao! Ambao wameishi eneo hilo maisha yao yote. 

MAMLAKA YA/WAKALA WA KURATIBU BEI ZA PANGO LA NYUMBA

Mheshimiwa Spika, kutokana na ongezeko kubwa la watu mijini, mahitaji ya nyumba za kupanga yamekuwa ni makubwa sana . Imekuwa ni jambo ka kawaida kwa wenye nyumba kujipangia bei za kodi ya nyumba kwa kadiri wanavyoona inafaa wao, kwa kuwa hakuna chombo cha kuwathibiti. Matokeo yake kodi ya nyumba imegeuka mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Kambi ya upinzani inaitaka serikali, iweke utaratibu utakaotambulika kisheria utakaoweka mwongozo na kuweza kuwadhibiti gharama za kodi za nyumba kwa ujumla wake. Kwa maana nyingine ni kuanzisha mamlaka ya udhibiti itakayoitwa ”Real Estate Regulatory Authority”.

WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI WA NYUMBA BORA NA VIFAA VYA UJENZI- (NHBRA)

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA), jukumu la Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (National Housing and Building Research Agency - NHBRA) ni kufanya tafiti, kuelimisha, kukuza, kushauri, kuhamasisha na kusambaza matokeo ya utafiti na utaalam wa ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu. Lengo la Wakala ni kuinua na kuboresha viwango vya nyumba kwa kutumia vifaa vilivyotafitiwa na vipatikanavyo hapa hapa nchini jambo ambalo litaongeza ubora wa maisha ya wananchi mijini na vijijini ili kutimiza malengo ya MKUKUTA. 

Mheshimiwa Spika,
 kambi ya upinzani inataka ipewe taarifa ni kwa namna na kiasi gani wakala huu umefanikiwa kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwani ujenzi wa nyumba za matope, fito na nyasi bado uko pale pale jambo ambalo linasababisha maisha bora kwa kila mtanzania kuwa ni kitendawili kwa miaka mingi ijayo!

MUHSTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAWAIDA NA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011


Mheshimiwa Spika,
Katika mwaka wa fedha 2010/11 , Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 53,848,061,000. Kati ya fedha hizo shilingi 6,423,295,000 zilitengwa kwa ajili ya mishahara, shilingi 25,159,688,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 22,265,078,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 


Mheshimiwa Spika, Hadi Mei , 2011 Wizara ilipokea jumla ya shilingi 27,787,178,679 (Bilioni 27.7)sawa na asilimia 51.5 ya tengeo la bajeti kwa mwaka. Kati ya fedha hizo, shilingi 25,658,017,495 sawa na asilimia 92.5 ya fedha zilizopokelewa , shilingi 13,226,897,075 zilitumika kwa ajili ya matumizi mengineyo, shilingi 8,499,539,334 zilitumika kulipa mishahara na shilingi 3,931,581,086 zilitumika kutekeleza miradi ya maendeleo.Kambi ya upinzani inaitaka serikali itueleze ni kwa sababu gani kati fedha za maendeleo zilizotengwa ( Tshs.22,265,078,000), zilizoweza kutumika ni Tshs. Bilioni 3.9 tu? Ni miradi mingapi iliyokuwa itekelezwe katika mwaka wa fedha 2010/2011 imeshindwa kutekelezwa kutokana na kukosekana huko kwa fedha?

POSHO NA MARUPURUPU VS FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani tulikuja na hoja ya kuitaka serikali iangalie upya mfumo wake wa ulipaji posho na marupurupu , lengo likiwa na kuisaidia serikali kuokoa matumizi yasiyo ya lazima na hatimaye fedha ambazo tunazitumia kulipana posho tuzielekeze kwenye matumizi yenye tija kwa wananchi. Tunashukuru kwamba hatimaye tulichokuwa tukikipigia kelele na kubezwa, kimeanza kutekelezwa na Serikali hii hii . Mhe. Waziri Mkuu wakati akiliomba Bunge kuahirisha hoja ya Wizara ya Nishati na Madini ili waende kujipanga upya alitamka yafuatayo , naomba kunukuu:“Mheshimiwa Spika, ushauri mlioutoa ni wa msingi sana. Moja mmesema Serikali nunueni mtambo na tusitafute visingizio vya fedha. Kwamba tafuteni kila mbinu huko,tafuteni,kateni posho zenu,kateni vitu gani,nendeni mkatazame magari mnayotumia haya, punguza huko. Tazameni OC yenu kikamilifu,mtaona kule ndani yako matumizi mengine ambayo mkiamua kwa dhati mnaweza kabisa mkayaondoa huko, yakaenda yakanunua mitambo ya uhakika,yakawasaidia hata kuongeza uwezo wa mafuta kwa ajili ya mitambo inayotumia mafuta” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika,
Kumbe inawezekana!Tukiamua kupunguza anasa na starehe na kuwekeza kwa wananchi wetu,inawezekana! Hakika Inawezekana!Katika Wizara hii zaidi ya shilingi bilioni moja, zimetengwa kwa ajili ya posho(wakati ni bilioni 3.9 tu zilitumika kwa shughuli za maendeleo). Cha kusikitisha zaidi hadi karne hii,kuna posho zinatengwa kwa ajili ya kuwalipia baadhi ya maafisa bili za maji na umeme ‘kwa maofisa wanaostahili’. Mfumo huu umesambaa mpaka kwenye Halmashauri zetu. 
Mheshimiwa Spika, ni wajibu wa serikali kuagalia upya mfumo huu wa kimwinyi, na kuacha huduma hizi ‘BINAFSI’ zigharamiwe kwa viongozi wa waandamizi (wakuu) tu, wa mihimili mitatu ya dola! Tatizo kubwa linalotukumba kama nchi, ni kuendesha mambo kwa mazoea. Lazima tubadilike! Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.
.................................................. ......
Halima James Mdee(Mb)
Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani-Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
15.08.2011




[1] Tathmini iliyofanywa na Consolidated Holding Corporation imegundua kwamba mwekezaji, RAI Group anayemiliki mashamba ya Setchet, Murjanda na Gidagamowd kati ya mashamba yanayolalamikiwa mwekezaji alikuwa amelima 53% tu ya shamba 
[2] Tarehe 29/1/2008 , akijibu swali Bungeni, aliyekuwa waziri wa kilimo kipindi hicho, Mhe. Wassira aliliambia Bunge kwamba jumla ya hekta 2500 zilikodishwa kwa vikundi vya ushirika vya wakulima wadogo 884Wassira aliliambia Bunge kwamba jumla ya hekta 2500 zilikodishwa kwa vikundi vya ushirika vya wakulima wadogo 884.
[3] Mwaka 2004 kupitia barua zenye kumbukumbu namba CAE/426/449/01 ya tarehe 14 Januari 2004 na barua yenye kumbukumbu namba GC.118/426/01 ya tarehe 22/7/2004 Wizara Chakula na kilimo iliiandikia Halmashauri ya wilaya ya Hanang ikiitaarifu juu ya uamuzi wa kamati ya Baraza la Mawaziri namba 8/2003 kilichofanyika Dodoma ,tarehe 10 Novemba 2003. Ambapo moja ya maamuzi ya hiko kikao ni kugawa mashamba ya warret na Gawal kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
[4] Hati ya kuandikishwa kwa Kijiji , na DSM VIJ. 7