Na Ramadhan Semtawa
MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amebainika kuwa na vijidudu 150 vya
malaria ambavyo vimemfanya alazwe Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji
Uangalizi Maalumu (ICU), katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wakati
Zitto akilazwa ICU ndogo (Min ICU), mbunge wa Viti Maalumu (CUF),
Claradiana Mwatuka, naye amelazwa katika kitengo hicho akisumbuliwa na
vidonda vya tumbo.Jana uchunguzi kuhusu Zitto ulibaini kuwa anasumbuliwa
na malaria kutokana na kuwa na wadudu hao ambao ni wengi kwa mtu kuweza
kuwahimili.Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jana wodini hapo
kuhusu hali yake, Zitto alisema kwa kifupi tu, "naendelea vizuri,
najisikia vizuri".
Awali, taarifa kutoka hospitalini hapo zilisema
Katibu Mkuu Wizara ya Afya alipiga marufuku Zitto kusumbuliwa na
kuagiza wote ambao walikuwa wakienda wasimsemeshe kwa muda mrefu wa
dakika 20.
Kwa upande wake, Msemaji wa hospitali ya Muhimbili,
Jezza Waziri, alisema Zitto baada ya kufanyiwa vipimo tangu alipofika
hospitalini hapo amebainika kuwa na vijidudu hivyo 150.Hata hivyo,
alisema uchunguzi zaidi kuhusu afya ya Zitto unaendelea na kuongeza
kwamba majibu ya vipimo zaidi yataonyesha kama kuna matatizo mengine au
la.
Alifafanua kuwa hadi sasa madaktari wamebaini tatizo kubwa
linalomsumbua mbunge huyo ni malaria na kuongeza kwamba jitihada na
taratibu zaidi za matibabu zimekuwa zikiendelea.
Kumpeleka India
Spika
wa Bunge, Anne Makinda jana jioni aliwaambia waandishi wa habari hapo
Muhimbili kwamba Zitto alikuwa akiendelea vizuri, lakini tatizo la
kichwa kuuma lilikuwa bado linamsumbua.Makinda ambaye alienda kumjulia
hali Zitto, alisema kutokana na tatizo hilo kuendelea, Ofisi ya Bunge
inafanya taratibu ili apelekwe India kwa uchunguzi zaidi.
Makinda
aliwataka Watanzania waendelee kumuombea ili aweze kupona.Taarifa za
watu wa karibu na Zitto zinasema kwamba huenda akasafirishwa kwenda
India kesho kwa ajili ya uchunguzi huo alioutangaza Spika Makinda.
Mbunge Mwatuka
Kuhusu
hali ya mbunge Mwatuka, Waziri alisema alifikishwa hospitalini hapo
juzi saa 4:00 usiku akisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo na
kwamba hadi jana alikuwa akiendelea na matibabu.Alifafanua kwamba,
mbunge huyo baada ya kufikishwa hospitalini hapo alianza kupatiwa
matibabu ambayo alisema yanaendelea vizuri.
Kaka wa Zitto
Kwa
upande wa kaka wa Zitto, Salumu Mohamed alifafanua kwamba kipindi chote
ambacho ndugu yake alikuwa Aga Khan haikuweza kubainika mara moja iwapo
ana wadudu 150 wa malaria.Hata hivyo, alisema baada ya kufika ICU
Muhimbili moja kwa moja alifanyiwa vipimo vya awali ambavyo
vilivyoonyesha kwamba alikuwa na kiasi hicho cha vijidudu.
"Baada
ya kufika hapa juzi alipelekwa moja kwa moja ICU na kuchukuliwa vipimo.
Matokeo ya awali, yanaonyesha ana malaria 150, hawa ni wadudu wengi
sana," alifafanua Kabwe.Alisema bado uchunguzi zaidi kuhusu afya ya
mdogo wake unaendelea kwani bado anasumbuliwa na tatizo la kuumwa na
kichwa.
Salum alisema kama kutakuwa na umuhimu wa tatizo hilo kwenda kutibiwa nje itafahamika na itafanyika hivyo.
Wodini alikolazwa
Isipokuwa
watu maalumu tu, watu wengine hawakuwa wakiruhusiwa kuingia alikolazwa
mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwani hata
waandishi wa habari waliofika hosipitalini hapo walizuiwa kuingia wodini
hapo.
Kulikuwa na utaratibu maalamu kwani hata kwa wale
walioruhusiwa walikuwa wakihojiwa kwanza, kwamba unatoka wapi na
unamfahamu vipi mbunge huyo ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).
Wabunge mbalimbali wakiwamo
Dk Hamis Kigangwallah wa Nzega na Dk Maua Daftari wakiwa na wafanyakazi
wengine wa Ofisi ya Bunge, walikuwa miongoni mwa waliofika wodini hapo
jana.
Friday, October 28, 2011
Friday, October 14, 2011
TAARIFA YA KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA AJALI YA MELI ZANZIBAR
Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi
wakuu wa kitaifa juuya tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice
Islanders-1, imemtaka Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano Hamad Masoud
Hamad kujiuzulu kwa hiyari yake kutokana na uzembe wa kutosimamia
majukumu yake aliyopewa na Serikali .
Akitoa taarifa juu ya Ajali ya Meli hiyo mbele ya Baraza la Wawakilishi leo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamza Hassan alieleza kuwa kutokana na uzembe huo uliofanywa na Wizara yake imeonyesha wazi kuwa Waziri huyo ameshidwa kusimamia ipasavyo majukumu yake aliyopewa na Rais.
Kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza Mamlaka ya Usafiri Baharini, kuna kipengele kinachomtaka Waziri kuunda Tume ya Uchunguzi pale linapotokea janga kama hilo lakini Waziri huyo alishindwa kuunda tume .
Aidha Mwenyekiti huyo alieleza kuwa Rais aliamua kuunda Tume wakati wajibu huo ulikuwa ufanywe na Waziri huyo mapema.
Kamati hiyo ilieleza kuwa inaamini kwamba kujiuzulu kwa Waziri wa miundo mbinu na mawasiliano kutapanua wigo wa demkrasia pamoja na uwajibikaji.
Kamati hiyo ilieleza kuwa kumetokea uzembe mkubwa kwa Nahodha wa meli hiyo kwa kushindwa kutoa taarifa mapema wakati meli ilipoanza kuingia maji hadi hapo abiria wenyewe kuanza kupiga simu wakiwa juu ya meli na inaanaaminika kwamba kama Nahodha angelitoa taarifa mapema basi abiria wengi sana wangeliokolewa wakiwa hai .
Mwenyekiti huyo alieleza kwamba kwa vile tukio hilo lilitokea usiku kama wangelipiga fataki kurusha angani ingelisaidia kutoa ishara kwa waokoaji kuona chombo kilipokuwa na kuweza kutoa msaada.
Kamati imeeleza kuwa kwa mujibu wa taratibu za meli yoyote ni lazima ziwe na vifaa vya kuokolea na mawasiliano ikiwemo fataki za kupiga angani pale inapotokea janga kama hilo.
Meli ya Mv Spice Islanders-1,ilitengezwa mwaka 1974 na kufanyiwa marekebisho makubwa nchini Ugiriki mwaka 200I.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 58,15 na upana wa mita 11.4 ilinunuliwa na Visiwani Shipping Company mwaka 2007 na kupatiwa usajili 2007 baada ya kufanyiwa ukaguzi kwa mujibu wa sheria na kuruhusiwa kuchukua abiria 600 na mizigo tani500.

Tuesday, October 11, 2011
Maulamaa wakijadili namna namna
![]() |
| Kutoka kushoto Maalim Rasuly Ramadhani, Uncle,Sheikh Kajanja kutoka Kigoma na Sheikh lutenant Shareef Hassan |
Saturday, September 17, 2011
Mpambano wa kukata na shoka kati ya Dar es salaam Zoofc na TaswaFc uliofanyika jana katika viwanja vya Dar es salaam Zoo kama unavyoonekana katika picha,mpambano huo wa kukata nashoka ulishuhudia timu ya TaswaFc ukishinda kwa taabu goli 3-0.
Dhumuni la mpambano huu ni ufunguzi wa viwanja vya michezo vilivyomo katika zoo hii pamoja timu ya Dar ZooFc na udhamini wa Dar zoo kwa TaswaFc.
Mchezo umechezeshwa na Mwamuzi wa kimataifa mstaafu othman Kazi, na Kamisaa akiwa Sakina Lioka.
Magoli ya Taswa Fc yalipachikwa na Majuto, Juma pinto na Hussein
Marketing Manager
Salim Hassan
Dar es Salaam Zoo
+255 784 524285
info@daressalaamzoo.com
www.daressalaamzoo.com

Thursday, September 08, 2011
SimbaSc Kidedea! Yanga waendelea kung'ang'ania mkiani
| Mshambuliaji "Hatari" wa Yanga Davis mwape akijaribu kuwatoka Mabeki wa Mtibwa |
Simba, ilichezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga, ilikuwa ya kusisimua muda wote.
Simba walianza mchezo kwa kulisakama lango la Villa, ambapo dakika ya saba, Gervais Kago, aliifungia bao hilo baada ya kuwatoka mabeki wa Villa na kuukwamisha mpira wavuni.
Villa Squad ambao wamepanda daraja msimu huu, walionesha uhai katika kila idara, lakini kosa walilofanya ni kushindwa kumdhibiti Kago.
Kipindi cha pili Villa Squad walirudi uwanjani na nguvu mpya, ambapo walilisakama lango la Simba mara nyingi, lakini washambuliaji walishindwa kufunga mabao.
Kwa matokeo hayo, Simba itakuwa imefikisha pointi tisa, ikiwa nyuma ya JKT Ruvu ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa sawa kwa pointi na Simba, lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wakati Simba wakizidi kuchanja mbuga, watani wao, Yanga, wameendelea kushikilia mkia baada ya kutoka suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar, anaripoti Ramadhan Libenanga, Morogoro.
Yanga ilicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Dakika ya 10, Jerryson Tegete wa Yanga, alimvisha kanzu beki Salum Swedi wa Mtibwa Sugar, lakini kipa Deo Munishi (Dida), aliuwahi mpira na kuudaka.
Davis Mwape wa Yanga, alipata nafasi nzuri dakika 13, lakini shuti lake lilimgusa beki wa Mtibwa na kuwa, ambayo haikuzaa matunda.
Dakika ya 30, Julius Mrope alipata nafasi nzuri baada ya kuwalamaba chenga mabeki watatu wa Mtibwa Sugar, lakini pasi yake fupi iliokolewa na mabeki.
Mtibwa Sugar walijibu mashambulizi dakika ya 42, kupitia kwa Thomas Morris, lakini shuti lake lilitoka nje ya lango.
Dakika ya 63, Kigi Makasi, alipiga shuti kali, ambalo lilitemwa na kipa wa Mtibwa, Dida, lakini Mrope alishindwa kuukwamisha mpira kimiani.
Kutoka Dodoma, timu ya Polisi Tanzania imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri, mjini Dodoma baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Ruvu Shoting
Wagombea CCM, Chadema wakwaa kisiki Igunga
Alisema kuwa mgombea wa CHADEMA Bw. Kashindye ni mfanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwa na
wadhifa wa Mkaguzi wa Elimu Wilaya ya Igunga, wakati mgombea wa CCM Dkt. Kafumu ni Kamishina wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Igumga Bw. Protace Magayane, alisema kuwa amepokea pingamizi hilo na anatoa nafasi kwa walalamikiwa kutoa vielelezo kabla hatua hazijachukuliwa.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Vijana Taifa wa CUF Bw. Mohamed Babu amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwao kuwa wao ni chanzo cha vurugu zilizosababisha mtafaruku wakati wa kurudisha fomu za wagombea wa Chama hicho na CHADEMA.
Alisema kuwa wafuasi wa CHADEMA ndio walikuwa wa kwanza kumzuia mgombea wa CUF Bw. Leopoad Mahona asiweze kurudisha fomu katika kipindi hicho ambacho na wao walikuwa wamejiandaa kurudisha fomu za mgombea wao.
Hata hivyo Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Igunga Bw. Christopher Saye alisema nao wamewasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD) wakidai kuwa walifanyiwa

Tuesday, September 06, 2011
Kesi dhidi ya Mbunge Lema yaanza kunguruma
| KESI ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya Chadema, Godbless Lema, jana ilianza kunguruma katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha kwa mawakili wa utetezi kuomba ifutiliwe mbali kwa madai kuwa walalamikaji hawana haki kisheria kupinga matokeo hayo. Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2010, imefunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaodai kuwa Lema alitoa lugha za kashfa na ubaguzi wa kidini na kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa chama chao, Dk Batilda Buriani. Walalamikaji hao wanadai kuwa lugha hizo ziliathiri matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Arusha Mjini.Wanaompinga Lema katika kesi hiyo ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo ambao kwa pamoja wanawakilishwa na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida. Wanadai kuwa katika siku na sehemu mbalimbali, Lema alidai kuwa Dk Burian, ameolewa Zanzibar na kwamba yeye na mumewe angekwenda kuishi visiwani humo baada ya uchaguzi. Wanadai kuwa Lema pia alitoa madai kuwa mgombe huyo wa CCM hakuwa mwaminifu na kwamba hiyo inadhihirishwa na kitendo cha kazaa na mwanamume mwingine. Mawakili wa utetezi Method Kimomogoro, anayemwakilisha Lema,ameweka pingamizi tatu na kumuomba Jaji Aloyce Mujuluzi kulitupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa walalamikaji wameshindwa kubainisha wanavyohusika na maneno yanayodaiwa kutamkwa na mteja wake dhidi ya Dk Burian. “Wadai hawana sababu za kisheria za kulalamika kwa sababu maneno wanayodai kutolewa kwenye mikutano ya hadhara (kama yalitolewa),yalilengwa kwa Dk Burian binafsi na si wao. Hawajaeleza madhara waliyopata wao kama wapiga kura,” alisema wakili Kimomogoro. Hoja hiyo ilimfanya Jaji Mujuluzi kumuuliza wakili huyo, “ina maana unalenga kusema pilipili usizokula zakuwashia nini,” Kwa upande wake wakili Kimomogoro alijibu kuwa ndiyo alikuwa na maana hiyo.Alitaja kifungu cha 111 (1) ya sheria ya uchaguzi inayoelekeza mdai au mlalamikaji katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi, kubainisha wazi makosa ya kisheria yaliyotendeka na madhara aliyopata, jambo ambalo alidai kuwa walalamikaji wameshindwa kufanya kupitia katika hati yao ya madai. Wakili huyo alisema kisheria wadai hawana haki kulamikia taratibu za kampeni kulingana na sheria ya maadili ya uchaguzi iliyosainiwa na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana. Alidai kuwa sheria hiyo inatoa nafasi kwa chama au mgombea pekee kuwasilisha malalamiko katika kamati ya uchaguzi ngazi husika ndani ya saa 48 tangu tukio lilipotokea. Kwa upande wao, mawakili wa serikali wanaomwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo, Timon Vitalis na Juma Masanja, waliunga mkono hoja za Kimomogoro na kwamba ushindi wa Lema, ulionyesha matakwa na maslahi ya umma hivyo wadai lazima waonyeshe yamewaathiri vipi. “Matokeo ya uchaguzi huonyesha matakwa ya walio wengi. Ili matokeo ya uchaguzi yatenguliwe, lazima wadai waonyeshe wameathirika vipi na hayo matokeo ambayo ni maslahi ya umma. Hati ya madai inaonyesha maneno yalitamkwa dhidi ya Dk Burian na si wao,” alisema wakili Vitalis akiomba shauri hilo litupwe. Alisema kifungu cha 111 cha sheria ya uchaguzi kinatoa haki kwa mpiga kura kupinga matokeo, lakini lazima azingatie sababu zinazoweza kusababisha matokeo kutenguliwa zilizoanishwa katika kifungu cha 108 cha sheria na kwamba hoja ya Dk Burian kuzaa na mwanamume mwingine haiangukii katika kifungu hicho bali inastahili kushughulikiwa kama kashfa binafsi. Baada ya upende wa utetezi kuwasilisha hoja za pingamizi, wakili wa wadai, Mugwai aliomba mahakama iwape muda wa kupitia na kujibu hoja, ombi ambalo lilikubaliwa na Jaji Mujuluzi. Baadaye, jaji huyo aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapoendela. |
STATE HOUSE REFUTES WIKI LEAKS ALLEGATIONS ON PRESIDENT KIKWETE
Director of Communications at the State House Mr Salva Rweyemamu speaks to the press flanked by Assistant Press Secretary to the President Ms Premmy Kibanga
PRESS STATEMENT
a. In an outrageous cable reported by Wikileaks, the former US Ambassador to Tanzania, Michael Retzer is reported to have said in his cable reports that President Jakaya Mrisho Kikwete has accepted gifts from the owner of the Kempinski Hotel chain, who is a citizen of the United Emirates.
b. This is, according to Ambassador Retzer, from a conversation he had with the Manager and Publicity Director of the former Dar es Salaam-based Kilimanjaro-Kempinski Hotel, Miss Lisa Pile.
c. This cable is as untruthful as it is outrageous. It is full of lies and innuendoes seeking to tarnish the good image and name of the President. It is unfortunate and highly disappointing that an ambassador worth his name could engage in this kind of lazy gossip.
d. The Directorate of the Presidential Communications would like to deny these lies in the strongest terms possible as follows:
2. We would like to state categorically that there has never been a time when the President received gifts from Ali Albwardy. This is definitely an outrageous claim and if there is evidence to the contrary, we would like to challenge Mr. Albwardy to produce it for the public to satisfy itself that what he is claiming are mere lies.
3. That there has never been a time, ever, when His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, during his time as Foreign Minister or currently as President of the United Republic of Tanzania, was flown by anybody to London on a subsidized shopping expedition to buy five suits. All his travels to London or any other places in the world have been duty assignments paid for by the Government of Tanzania. The matter of him being flown to London for subsides shopping of five suites is outrageous.
4. That during his entire life, as Foreign Minister or as President, the President has never met in London nor travelled with Ali Albwardy to London on a shopping expedition.
5. That the President was not responsible for raising nor receiving campaign funds for CCM Party during the 2005 General Elections. He was simply the flag bearer of the Party. However, he is privy to information that Kempinski Kilimanjaro Hotel was never asked nor contributed a single cent towards CCM campaign. Therefore the allegations that Kempinski Kilimanjaro Hotel contributed one million (USD 1,000,000) toward CCM campaign are baseless and unfounded.
6. That the Government permission for possessing of the Kilimanjaro Hotel by Kempinski Hotels and the subsequent permission to Kempinski to build two new hotels - one on the edge of the Ngorongoro Crater and another on the Serengeti plains overlooking the main animal migration routes were issued by the Third Phase Tanzania Government and not by Mr. Kikwete’s Administration.
7. However, President Kikwete declined to grant Kempinski Hotels permission to build on the Ngorongoro Crater on the strength of environmental concerns. How come then that the President who has been offered so many favors such as suits and election money, took this principled position? This therefore testifies to the fact that, claims that the President has received favours are with malice intentions from his authors.
8. That it is a lie that Mr Kikwete has frequented Kilimanjaro Kempinski Hotel in his personal capacity. The records are very clear; the President has never, ever on his own visited that Hotel except on official duties or when he has escorted official state guests.9. It is unfortunate that the distinguished Ambassador would believed and transmit such baseless lies and ear-says from a single source. The Office of the President takes strong exception to such behaviour which seeks to tarnish the name and person of the President.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,Dar es Salaam.
INVITATION TO THE WORLD TOURISM DAY EXHIBITIONS IN TANZANIA: MNAZI MMOJA GROUNDS: FRIDAY 30TH SEPTEMBER TO SATURDAY 1ST OCTOBER 2011
Dar es Salaam Tourist Executive Board (DTEB) is the coordinator of this year’s World Tourism Day.The World Tourism Day (WTD) is a renowned public awareness day designed by the United Nations World Tourism Organization (UN-WTO) and celebrated on 27 September of every year. The WTD Celebration is an effective way of public awareness creation of the importance of tourism and a stimulant to development activities that promote the benefits derived from tourism. Stake holders spearheading the celebration of WTD 2011 in Tanzania are Ministry of Natural Resources and Tourism which is the Tanzania Country desk office of Tanzania’s membership to UN on matters relating to Tourism, Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) through the Cluster Competitive Programme (CCP), Tanzania Tourist Board (TTB), Tanzania Confederation of Tourism (TCT), Dar es Salaam Tourist Executive Board (DTEB, The Dar es Salaam City Council and the Dar es Salaam Regional Commissioner who is the host of the celebration.In Tanzania the socio economic importance of tourism has been growing from strength to strength resulting in creation of jobs from cities to rural areas and generating considerable foreign income to the nation and to individuals. This is the third time for Tanzania to celebrate WTD at the national level. The other celebrations were held in Bukoba 2006 and in Iringa 2009. Activities to mark the event will include a speech by the Minister of Natural Resources and Tourism on 27th September 2011, Exhibitions on tourism and culture on 30thSeptember and 1st October 2011 as well as Tourism as a potential hungry market for produce from primary producers of horticulture and food processing, There will also be round table discussions and Gala dinner scheduled for 1st of October 2011. Other planned activities expected to run parallel to these events include the launching of DTEB Tourist Information Centre at the Julius Nyerere International Airport and a float around streets of Dar es Salaam.We call for your highly valued supportAs a stakeholder in the tourism industry in Tanzania, we are extending to you an invitation to be part of this initiative and humbly request you to consider participating in these celebrations. We wish your esteemed company to be one among many companies and organizations which will be showcasing their products and services during the World Tourism Day exhibitions scheduled for Friday 30th September to Saturday 1st October 2011 at the Mnazi Mmoja grounds, Dar es Salaam.Exhibition fee for the two days amounts to Tzs. 500,000 (Five hundred thousand shillings only) which will cover for one booth size (3 × 3 meters) provided with one table and two chairs. Additionally as a strategy to promote your products and services to the general public countrywide, the organizing committee is arranging for a two weeks 30 minutes a day Television program to be broadcasted on prominent TV stations during prime times (between 6:00 PM and 10:30 PM) from 27th September to 6th October 2011. For your company to feature in this TV program you are requested to contribute Tzs. 500,000 (Five hundred thousand shillings only) and you will receive 5 minutes of the program to talk about your business and showcase your products and services to your existing and potential customers countrywide. Recording and interviews regarding your company and products must be done earlier and we would appreciate your prompt confirmation to be part of the program before 20th September 2011.Kindly note that all payments should be directed/ addressed to the following Account:Account Name: Emerging Markets Group (T) LtdBank Name: Stanbic BankAccount USD 2: 0240011905601Account TZS 3: 0140011905602We hope you will reflect on this plea and decide to join hands with us in pushing the tourism industry in our country forward.For more details please contact:Paul R.K Mashauri, PresidentThe East Africa Speakers BureauOff: Mikocheni B Area, Plot # 320,Off Old Bagamoyo Road Dar es Salaam +255 2700051 +255 717 653544/ +255 684005839 mashauri@eastafricaspeakers.net mashauri@printmediatz.com
Friday, September 02, 2011
The Dk. Remmy Ongala Foundation is a charitable organisation, founded by Remmy’s daughter, Aziza Ongala, in memory of her father — an outstanding Tanzanian popular musician and social campaigner.http://www.thedkremmyongalafoundation.com
Tuesday, August 30, 2011
EID MUBARAQ
Hello Tanzanian!
We would like to share Eid Mubarak to all of you and welcome all of you to share with us Eid celebration at our attractive zoo at affordable cost for your enjoyment.
Dar es Salaam Zoo has now established seven (7) spacious gardens with adequate day time accommodation to hold Group/Family Celebrations at reasonable costs. This is apart from the pleasure of enjoying the natural fresh environment, the direct interaction with wildlife and the excitement of recreation celebrities provided at the zoo such as horse/camel riding and motor cycle/go-cart racing in and outdoor games like football, tennis and volleyball . We just open u horse club with affordable fee to be a membership .
Salim Hassan
Marketing Manager
info@daressalaamzoo.com
Friday, August 26, 2011
Walipa Kodi 15 Bora
Mheshimiwa Spika,
1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:
i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);
iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);
iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);
v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);
vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);
vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);
viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);
x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);
xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);
xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);
xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);
xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na
xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).
2. Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria

Zitto aibua tuhuma nyingine dhidi ya Serikali
SERIKALI na Bunge zimeingia katika mkwaruzano mwingine baada ya Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, kuituhumu Serikali kuwa imemsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi (CHC), Mathusela Mbajo, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuvujisha siri za Serikali kwa Bunge.
Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa tuhuma hizo jana wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2011/2012.Juzi Bunge liliingia katika mvutano na Serikali baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo, bila Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kujadiliwa bungeni.
Kabla sakata hilo halijapoa, Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alidai kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya Mbajo ni matokeo ya Azimio lililopitishwa na Bunge kuliongezea shirika hilo muda.
"Baada ya kufanya marekebisho hayo, azimio lililopelekwa na Serikali bungeni likiwa na nia ya kuunganisha shirika hilo na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Zitto alisema uamuzi huo wa Bunge haukuwafurahisha baadhi ya watendaji wa Serikali hivyo ikaamuliwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu huyo wa CHC, kwa tuhuma zilizojaa majungu kutoka kwa wanaojiita wafanyakazi wa CHC," alisema Zitto na kuongeza.
"Tuhuma hizo ziliwasilishwa kwangu binafsi na kunakiliwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Kufuatia maagizo ya Waziri wa Fedha kwa Bodi ya Wakurugenzi wa CHC, Mtanzania huyu akasimamishwa kazi na CAG ameombwa kuchunguza majungu yale kutoka kwa wanaojiita wafanyakazi wa shirika hilo.
"Mheshimiwa Spika, nilikuandikia barua kukuomba hatua mwafaka zichukuliwe, kwani suala hili bado lipo katika mamlaka ya Bunge na kwa mujibu wa Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sheria namba 3 ya mwaka 1988, uamuzi huu Waziri wa Fedha ni sawa na kulidharau Bunge"
Waziri kivuli huyo aliongeza: "Barua ya wanaojiita wafanyakazi wa CHC (niliyoandikiwa Juni 24, 2011, siku mbili tangu kupitishwa kwa azimio la Bunge na kuwatuhumu mawaziri kuwa walishawishiwa), Barua ya maelekezo ya Serikali (iliyosainiwa na ndugu Mmbaga, Msaidizi wa Waziri Mkuu ya tarehe 10 Agosti 2011) na barua yangu ya majibu (18 Agosti 2011) niliyowapa, zimewasilishwa mezani kwako kama vithibitisho na kwa hatua zaidi utakazoona inafaa."
Zitto aliliomba Bunge kusimama imara ili kuzuia kuingiliwa kwa mamlaka yake na tawi la utendaji kwa kuwa mijadala ndani ya Bunge inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo lisipokuwa makini Bunge litaendelea kudharauliwa hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia Serikali ipasavyo.
"Ninataka maelezo ya kina ya Waziri wa Fedha kwa nini amechukua hatua nilizoeleza hapo wakati akijua jambo hili lipo mezani kwa Spika wa Bunge."
Usimamizi wa mashirika ya Umma
Katika eneo hilo, Zitto aliituhumu Serikali kwa kushindwa kusimamia hisa zake katika makampuni akieleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) imekuwa dhaifu mno katika kusimamia mali za umma katika mashirika na kutoa mfano wa hisa za kampuni ya Oryx na Tigo.
"Kampuni ya Oryx ilikuwa inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 50 mpaka mwaka 2004. Mwaka 2004, kupitia ofisi ya TR Serikali iliuza hisa zake ambazo ni asilimia 50 kwa bei ya kutupa kwa thamani ya dola 2.5 milioni. Hivi sasa Oryx ni moja ya kampuni inayofanya vizuri sana katika sekta ya mafuta, lakini hatuna umiliki tena na pesa kiduchu tulizopata zimekwishatumika," alisema Zitto na kuongeza:
"Pia Serikali ilikuwa na hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel ambayo kwa sasa inajulikana kama “tigo”. Katika hatua ya kushangaza Serikali imeuza hisa zake asilimia 16 kwa thamani ya Dola 1.3 milioni mwaka 2006 na kwa sasa kampuni hiyo ni ya kigeni kwa asilimia mia moja jambo ambalo ni kinyume na sheria."
Zitto alisema kampuni za simu zinatakiwa kumilikiwa na Watanzania si chini ya asilimia 35.
Makusanyo ya kodi
Zitto alisema kambi ya upinzani nasikitishwa na pungufu ya makusanyo madogo ya kodi na kwamba, hali hiyo imetokana na Serikali kushindwa kusikiliza maoni yanayotolewa na kambi hiyo kila mwaka ambayo ni vyanzo mbadala vya kuongeza mapato.
Kuhusu bei ya dhahabu
Zitto alifafanua kwamba bei ya dhahabu katika soko la dunia imeongezeka mara dufu na hadi kufikia Agosti 23, mwaka huu. Kwa mujibu wa mtandao wa gold-alert bei ya dhahabu ilikuwa Dola za Marekani 1,902.61.
Alisema hilo ni ongezeko kubwa na hivyo kuna haja ya kuangalia namna ya kurekebisha kodi kwenye madini hayo ili taifa lifaidike na bidhaa hiyo.
Kutokana na ongezeko hilo la bei, alisema kambi ya upinzani inaitaka Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) kuanza mara moja kufanya utafiti wa namna bora ya kutoza kodi ya faida kwenye dhahabu (windfall tax), ili kuongeza mapato ya Serikali kwa sababu wawekezaji wanapata faida mara dufu kwa sasa.
"Matokeo ya tafiti hii yaletwe bungeni kama muswada wa sheria ili kurekebisha sheria za kodi na kutoza aina hii mpya ya kodi," alisema Zitto
Alisema kambi ya upinzani inapendekeza kwa kuwa gharama ya kuzalisha wakia moja ya dhahabu hapa nchini ni wastani wa dola za marekani 650, basi bei ya dhahabu ikiwa ya kati ya dola 1,000 – 1,300, mrabaha uwe mara mbili ya tozo za sasa.
"Kwa mfumo huu, taifa litafaidika na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia na pale ambapo bei zitashuka wawekezaji watalipa mrabaha wa kawaida," alifafanua aziri kivuli huyo.
Alisema iwapo mfumo huo wa kodi katika madini ungekuwa unatumika sasa na ambapo bei ya dhahabu imefikia zaidi ya dola 1,900 kwa wakia, na nchi inazalisha takribani tani 60 ya dhahabu kwa mwaka, Serikali ingekusanya takribani Sh450 bilioni kama mrabaha.
"Hii ingetuwezesha hata kutokopa kwa ajili ya umeme wa dharura kama tunavyoelekea kufanya sasa."

Monday, August 22, 2011
ASEMA KAMA INATAKA KUENDELEA KUSHIKA DOLA IWAFUKUZE WATUMUMIWA WA UFISADI
| WAZIRI Mkuu mstaafu, John Malecela amekitaka Chama chake cha Mapinduzi (CCM) kuwachukulia hatua za haraka wala rushwa walioko ndani yake kuanzia ngazi ya juu hadi chini kama kinataka kuendelea kushika dola.Kauli ya Malecela ambaye ni Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, inakuja kipindi ambacho mpango mkakati wa chama hicho wa kujivua gamba unaonekana kupigwa kalenda. Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Sea View, Upanga Dar es Salaam jana, Malecela alisema ni muhimu wala rushwa wakaondolewa haraka bila kucheleweshwa ili chama kiendelee kuwapo. Malecela alinukuu maandiko ya Mungu katika Ukristo akisema: "Mimi ni Mkristo, maneno ya Mungu yanasema ukiwa na jicho bovu na ukiona linakuzuia kuingia mbinguni litoe ili uweze kuingia." "Kama kuna corrupt people in the party (wala rushwa ndani ya chama), ni kuwaondoa ili CCM iendelee kuwapo." Hata hivyo, alisema suala la kujivua gamba haliwezi kuwa kwa watu wanne au watano, bali chama kisafishe wala rushwa wote waliopo ndani yake kuanzia ngazi ya juu hadi chini. Kujivua gamba Mpango wa kujivua gamba kwa CCM ulianza kutangazwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa chama hicho yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni akisema yalikuwa na lengo la kukihuisha. Rais Kikwete alisema chama hicho kiliwahi kufanya mabadiliko mbalimbali kuanzia TANU kwa lengo la kujisafisha na kujipanga upya, baada ya kujifanyia tathmini kuhusu mwelekeo wake kwa wakati husika. Mpango huo baadaye ulijadiliwa katika CC iliyokutana Mjini Dodoma mnamo Aprili ambayo pamoja na mambo mengine utekelezaji huo ulianza kwa Kamati hiyo Kuu kujiuzulu yote na kusukwa upya huku baadhi ya watuhumiwa akiwamo Andrew Chenge kutupwa nje. Katika kikao hicho, ilitangazwa watuhumiwa wa ufisadi ukiwamo wa Richmond, Rada na Kagoda iliyochota Sh40 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wangepaswa kujipima na kuachia nafasi zao ndani ya siku 90 lakini hadi kikao cha CC cha mwezi uliopita, watuhumiwa hao walikuwa hawajajiuzulu. Badala yake, CC ilitoa muda zaidi kusubiri uamuzi wa kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho inayotarajiwa kukutana mwezi ujao.Hata hivyo, hakuna dalili zozote za watuhumiwa wakubwa wanaotajwa katika kashfa hizo za rada na Richmond kujiuzulu huku chama kikionekana kuwa katika wakati mgumu kuwafukuza, huku hatua ya kutowafukuza ikitajwa kama kitanzi kinachoweza kukimaliza kisiasa. Tuhuma za kumiliki shamba hekta 100 Akizungumzia madai yaliyotolewa Bungeni hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kwamba anamiliki hekta 100 za shamba huko Mvomero, Morogoro, Malecela alisema hana habari juu ya umiliki huo akisema: "Sina hati yake na wala sijawahi kufika kuliona, hata sijui liko sehemu gani ya Mvomero." Alisema wakati Serikali ilipoipa Mvomero hadhi ya wilaya, iliwapa baadhi ya viongozi mashamba ili waendeleze maeneo hayo au wavute wawekezaji katika wilaya hiyo."Mimi niliambiwa nimepewa hekta 100 lakini sijawahi kufika kwenye eneo hilo, hata hati ya shamba hilo sina hivyo ni kusema sina shamba Mvomero." "Ambaye analitaka shamba hilo akalichukue au kama kuna mtu anayefikiri kuwa ana hati ya shamba hilo aende wizarani athibitishe." "Ni miaka 10 imepita tangu niambiwe suala hilo, wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akiwa ni (Samwel) Kamote, lakini sheria za kutoendeleza mashamba si zinajulikana kama lipo tu kwa nini lisichukuliwe?" Malecela alisema asingeweza kupeleka trekta kutoka Dodoma kwenda kulima Mvomero hekta 100 kwa kuwa uwekezaji unahitaji zaidi ya hekta 300. Alichokisema Mdee bungeni Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), akisoma bajeti mbadala ya upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2011/12 aliwataja baadhi ya viongozi wa CCM wakiwamo Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa akiwatuhumu kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi mkoani Morogoro huku wakishindwa kuyaendeleza. Hata hivyo, Mkapa anaelezwa kuendeleza shamba lake. Katika orodha hiyo pia ametajwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula, aliyekuwa Naibu wake (Tanzania Bara), Hassan Ngwilizi na Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawab Mulla. Mdee alisema umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi unawanyima fursa wananchi wa kawaida kupata maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza kwamba, vigogo hao kwa kutumia nafasi zao waliwanyang’anya wananchi ardhi hiyo na kujimilikisha wenyewe lakini kwa sehemu kubwa wameshindwa kuyaendeleza. “Mheshimiwa Spika, matatizo ya ardhi kwa wakubwa kunyang’anya wanyonge imekumba pia Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambako mgogoro huu unakumba shamba namba 299 iliyokuwa Narco Ranches lenye ukubwa wa hekta 49,981," alisema na kuongeza: “Taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa maeneo yaliyokuwa yamepangwa kugawiwa kwa wanavijiji wa Kijiji cha Wami, yamegawiwa wanavijiji wafuatao,’’ alisema na kuanza kuwataja vigogo hao kwa majina mmoja baada ya mwingine. Akitoa orodha hiyo, Mdee alisema Mangula anamiliki hekta 2,000, Mwinyi hekta 2,000 na Mkapa hekta 1,000 ambaye hata hivyo, ndiye pekee aliweza kuliendeleza shamba lake. Katika orodha ya Mdee alimtaja pia Sumaye kwamba anamiliki hekta 500, Malecela hekta 100 na Ngwilizi ambaye anamiliki hekta 100 huku akisisitiza orodha hiyo ni ndefu.Mdee alitaka Serikali itoe maelezo kwamba ni vigezo vipi vilitumika kuwagawia ardhi viongozi hao huku wakiwanyima ardhi wananchi wa maeneo husika. |
Jembe jipya darajani
Matajiri wa londo Chelsea fc wamekubaliana na Mchezaji Juan Mata pamoja na Club ya valencia ya Uhispania ada ya Uhamisho ya Pound 26ml na kumnyakua mchezaji huyo kwa ajili ya msimu huu wa ligi.
![]() |
| Wambea tafuteni Kivuri Jua kali Mwaka Huu |
Mtu Mweusi Mboga Asia
ONYO - Nimepata kwa email. Kama huna roho ngumu usiangalie hizi picha! Kama sikosei ni Thaliand hapo. Cheki wanavyomkata huyo marehemu kama nyama kwenye bucha! Nadhani tumejua ndugu zetu walioenda huko na wakapotea waliishia wapi sasa! DUH!
Email Text:
THAI & CHINESE PEOPLE EATING A BLACK MAN. I have never seen anything like this before! The Asian appetite for "exotic" taste sometimes scare me - from stories of cat eating to dogs, to lizard, snakes to all sorts of crazy fish, then human embryos and now to fully grown humans! The photo of the person you are about to watch could have been somebody's fiance, husband or Dad! This looks too real to be true.
How I wish all black leaders watch these photos and give guidelines of who they allow to migrate into their countries. The time has come for black (Africans, American, West Indies etc) to rise and unite together against attrocities committed by foreigners on them either on their soil or abroad. Time to pray to God is now!

Labels:
Che Mponda
Subscribe to:
Posts (Atom)