Thursday, September 08, 2011

SimbaSc Kidedea! Yanga waendelea kung'ang'ania mkiani

Mshambuliaji "Hatari" wa Yanga Davis mwape akijaribu kuwatoka Mabeki wa Mtibwa
MABINGWA wa Ngao ya Jamii, Simba, jana iliendeleza ubabe katika mechi za Ligi Kuu Bara, baada ya kuchapa Villa Squad bao 1-0.Mechi hiyo ya tatu kwa
Simba, ilichezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga, ilikuwa ya kusisimua muda wote.

Simba walianza mchezo kwa kulisakama lango la Villa, ambapo dakika ya saba, Gervais Kago, aliifungia bao hilo baada ya kuwatoka mabeki wa Villa na kuukwamisha mpira wavuni.

Villa Squad ambao wamepanda daraja msimu huu, walionesha uhai katika kila idara, lakini kosa walilofanya ni kushindwa kumdhibiti Kago.

Kipindi cha pili Villa Squad walirudi uwanjani na nguvu mpya, ambapo walilisakama lango la Simba mara nyingi, lakini washambuliaji walishindwa kufunga mabao.

Kwa matokeo hayo, Simba itakuwa imefikisha pointi tisa, ikiwa nyuma ya JKT Ruvu ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa sawa kwa pointi na Simba, lakini zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Wakati Simba wakizidi kuchanja mbuga, watani wao, Yanga, wameendelea kushikilia mkia baada ya kutoka suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar, anaripoti Ramadhan Libenanga, Morogoro.

Yanga ilicheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Dakika ya 10, Jerryson Tegete wa Yanga, alimvisha kanzu beki Salum Swedi wa Mtibwa Sugar, lakini kipa Deo Munishi (Dida), aliuwahi mpira na kuudaka.

Davis Mwape wa Yanga, alipata nafasi nzuri dakika 13, lakini shuti lake lilimgusa beki wa Mtibwa na kuwa, ambayo haikuzaa matunda.

Dakika ya 30, Julius Mrope alipata nafasi nzuri baada ya kuwalamaba chenga mabeki watatu wa Mtibwa Sugar, lakini pasi yake fupi iliokolewa na mabeki.

Mtibwa Sugar walijibu mashambulizi dakika ya 42, kupitia kwa Thomas Morris, lakini shuti lake lilitoka nje ya lango.

Dakika ya 63, Kigi Makasi, alipiga shuti kali, ambalo lilitemwa na kipa wa Mtibwa, Dida, lakini Mrope alishindwa kuukwamisha mpira kimiani.

Kutoka Dodoma, timu ya Polisi Tanzania imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri, mjini Dodoma baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Ruvu Shoting

No comments: